HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 December 2017

KAMPENI YA UZALENDO NA UTAIFA 'NCHI YANGU KWANZA' KUZINDULIWA NA WIMBO MAALUM

Wasanii wa muziki wakiongozwa na msanii wa muziki wa asili, Mrisho Mpoto wameandaa wimbo maalumu ambao utaimbwa Usiku wa Kitendawili katika uzinduzi wa kampeni ya Uzalendo na Utaifa ‘Nchi Yangu Kwanza’ inayotarajia kufanyika siku ya kesho huko mkoani Dodoma.

Kampeni hiyo itazinduliwa na Rais John Pombe Magufuli na baada ya hapo itazunguka katika mikoa mbalimbali nchini kuhamasisha masuala ya Uzalendo.

Akiongea na waandishi wa habari Alhamisi hii, mmoja kati ya waratibu wa kampeni hiyo, Mrisho Mpoto amesema wimbo huyo umeandaliwa na wasanii wengi akiwemo Witness ‘Kibongwe Mwepesi’ pamoja na wasanii wengi likuki waliojaliwa vipaji.

“Wasanii kama wasanii tuliona tukae chini tuandae wimbo kuonyesha suala la uzalendo ni kitu muhimu kwa ustawi wa taifa, bila uzalendo hakuna amani. Tuunge juhudi za Rais wetu Magufuli kwa sababu ameonyesha kwamba yeye ni mzalendo wa kweli na ameonyesha kuwa yeye anaweza kufanya mambo makubwa kwaajili ya watanzania wa chini,” alisema Mpoto.

Muimbaji huyo alisema Kampeni hiyo ya Kitaifa itakuwa ikifanyika kila mwaka sambamba na maadhimisho ya kifo cha Baba wa Taifa, Hayati Julis Kambarage Nyerere.

Kwa upande wa Witness alisema yeye kama msanii wa kike anajisikia fahari kuimba uzalendo kwaajili ya nchi yake.

“Uzalendo ndio kila kitu katika maisha ya binadamu na usalama wa nchi yake, ukiona kitu kibaya kinawanyemelea watanzania unatakiwa kupaza sauti kwa sababu ni watu wako, uzalendo ni uchungu wa ndani kwaajili ya nchi yako. Kwahiyo huu wimbo utaenda kufungua njia na pia kutoa elimu kwa sababu kuna baadhi ya watu hawajui uzalendo ni kitu gani,” alisema Witness.

Mrembo huyo wa muziki alisema watanzania wanatakiwa kujitokeza kwa wingi usiku huo ili kusikia madini ya viongozi wao pamoja na wazee ambao watapata fursa ya kusimulia hali ya uzalendo katika ujana wao ilikuwaje

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad