HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 8 December 2017

Mkazi wa Arusha ashinda milioni 86 ya M-bet

Mkazi wa Arusha, Sagi Thomas (37) amejishindia kitita cha sh milioni 86 kwa kubashiri kwa usahihi mchezo maarufu kwa ‘Perfect 12’ unaondeshwa na kampuni ya mchezo wa kubahatisha ya M-Bet.

Thomas alikabidhiwa kitita chake jana na Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley. Malley alisema kuwa Thomas alifanikiwa kubashiri sahihi jumla ya mechi 12 kati ya 17 na kuwa mshindi wao wa droo ya 17 tokea kuanzishwa kwa mchezo wa Perfect 12. Alisema kuwa serikali imejipatia jumla ya Sh milioni 15.5 kutoka kiasi hicho cha fedha ambacho ni asilimia 18 kwa mujibu wa sheria.

“Kama tulivyosema hapo awali, M-Bet ni nyumba ya washindi na leo tumedhihirisha usemi wetu ambapo Thomas anajisindia mamilion ya fedha kwa kutumia kiasi cha She elfu moja tu, hii imedhihirisha kuwa tunawaomba mashabiki wa soka kuendelea kucheza mchezo wetu ili kujishindia fedha,” alisema Malley.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Thomas alisema kuwa atazitumia fedha hizo kwa kuanzisha vitega uchumi na vilevile kuwaendeleza kielimu ndugu zake.

“Nina furaha sana, mimi ni mwajiriwa wa serikali, leo hii nina faraja kubwa kuona kiasi cha Sh 1,000 tu kimeniwezesha kushinda mamilioni ya fedha, M-Bet imebadilisha maisha yangu” alisema Thomas. Meneja wa Tehama wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Kabora Mboya aliwashukuru M-Bet kwa kuendelea vyema na shughuli zake mbali ya kuwazawadia washindi mara kwa mara.
 Afisa Habari wa Kampuni ya M-Bet, David Malley (kushoto) akimkabidhi hundi mshindi wa mchezo wa Perfect 12, Sagi Thomas (kulia) ambaye amejishindia kitita cha sh milioni 86. Katikati ni Meneja wa Tehama wa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), Kabora Mboya.
 Mshindi wa mchezo wa Perfect 12 Sagi Thomas 'akipozi' na mfano wa hundi mara baada ya kukabiziwa jana. Kalinga alijishindia kitita cha sh milioni 86.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad