HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 8, 2017

Waziri Mwakyembe awapa kazi wasanii ya kufundisha Uzalendo


Waziri wa habari utamaduni sanaa na michezo Dr. Harrison Mwakyembe amekutana na wasanii wa tasnia mbalimbali hapa nchini na kumzungumza nao juu ya ujio wa Kampeni ya Uzalendo na Utaifa 'Nchi Yangu Kwanza' inayotarajiwa kuzinduliwa Disemba 8 mwaka huu huko mkoani Dodoma.

Waziri huyo aliwataka wasanii kuendeleza na kuutangaza uzalendo wetu unaoendana na maadili yetu, ikiwa kauli mbiu ni 'Nchi Yangu Kwanza'.

Waziri huyo amesema hayo jijini Dar es Salaam katika ukumbi wa uwanja wa Taifa akiwahimiza Wasanii hao ambao
 ni kioo cha jamii kuwa na mchango mkubwa katika kuijenga nchi yetu.

'Mrisho ndiye aliyesababisha sisi kuwa hapa, alileta wazo na sisi 
tumelishughulikia na sasa hivi limekuwa wazo kubwa hata mwenyewe haamini. Kwahiyo sisi tumewaita hapa kwaajili ya kampeni hii ambayo inakwenda kulikomboa Taifa letu. Waandishi wa habari pia ni miongoni mwa mashujaa wetu waliotufikisha hapa tulipo" amesema waziri Mwakyembe.


Waziri Mwakyembe amesema kuwa siku ya Ijumaa 8, Desemba mwaka huu Dodoma kutakuwa na uzinduzi rasmi wa kampeni ya uzalendo kwanza kwa nchi yangu ambapo uzinduzi huo utahudhuruwa na Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli akiwa ni mzalendo wa kwanza katika ujenzi wa taifa letu.

Aidha Naibu Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na michezo Juliana Shonza amesikitishwa na baadhi ya wasanii ambao ni vioo vya jamii hapa nchini kutokuwa na maadili ya kizalendo kwa kutumia vibaya vyombo vya mawasiliano kwa kupiga picha zisizofaa na kutuma kwenye mitandao ya kijamii,Na amewataka kuwa mabalozi wazuri katika kutangaza uzalendo kwanza Hapa nchini

Msanii Mrisho Mpoto akizungumza na na wasan wenzake mbele ua Wwziri wa habari,Utamaduni,Sanaa na mMichezo Harrison Mwakyembe pamoja na Naibu waziri Juliana shonza.
Hata hivyo naibu huyo ametoa pongezi za dhati kwa Mrisho mpoto akiwa mzalendo alietoa wazo hilo na wasanii wenzake, Na amesema kuwa wizara imeipa uzito kampeni hii na kuamua kuwa inde mkoani kwaajili ya uzinduzi
 huo.

Vile vile pia naibu Shoza amempongeza mwanamashumbwi Ibrahim class kwa kuwa mzalendo kwa kuwa bingwa wa 3 barani Afrika na asie na 
mpinzani nchini Tanzania na kumkabidhi hundi ya shilingi milioni 18 laki 2 na 40 elfu.

Nae bondia Ibrahimu class amemalizia kwa kusema kuwa mazoezi na kujiamini ndio kinachomfanya afanye vizuri katika mashindano yake ya ndani na nnje ya nchi na ametoa shukrani zake za dhati kwa watanzaia kwa kumuunga mkono katika mapambano yake.
Waziri Mwakyembe awapa kazi wasanii ya kufundisha Uzalendo

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad