HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 22 December 2017

NAIBU SPIKA AKABIDHI MISAADA MBALIMBALI WILAYANI RUNGWE

Naibu Spika Dk Tulia Ackson amefanya ziara katika baadhi ya maeneo Wilayani Rungwe mkoani  Mbeya ikiwa ni kutekeleza baadhi ya ahadi alizowahi kuzitoa katika kusaidia maendeleo, kwanza alianza kwa kutoa vifaa vyenye thamani ya shilingi milioni tano katika shule ya sekondari Bujela
 Akizungumza katika shule ya  Bujela Dk. Tulia amesema  kuwa  ahadi lazima zitekelezwe jambo  ambalo hata Rais  Dk. John Pombe Magufuli i husisitiza kutoigiza  siasa kwenye mambo ya maendeleo.

"Leo kama  Tulia Trust  tuliahidi vifaa vyenye thamani ya Milioni tano na tayari tumetekeleza kwa kuja navyo vikiwemo bati, mbao, mchanga, saruji, chokaa, rangi, vioo, nondo .amesma  Dk Tulia"
 Amesema kufanya hayo  yote ni kwa ajili ya kuhakikisha tunawatengenezea watoto wetu mazingira mazuri ya kujisomea na baadae watuletee maendeleo sisi wazazi wao hivyo niwaombe viongozi wote tushikamane.
Katika ziara yake hiyo alitembelea  Kanisa la Bujela ambalo liliharibiwa na upepo uliosababishwa na mvua huko  ambapo Dk.Tulia alichangia jumla ya mabati 100 yenye thamani zaidi ya milioni mbili Kwa ajili ya kukamilisha ukarabati wa kanisa hilo ambalo tayari ujenzi wake ulianza kwa jitihada za waumini wenyewe kuchangishana.

Aidha Dk.Tulia aliwahimiza waumini pamoja na viongozi wa dini kuendelea kuliombea taifa la Tanzania amani pamoja na kumuombea Rais Magufuli ili aendelee kuiongoza nchi salama.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad