HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, December 22, 2017

DK NDUGULILE AZINDUA PROGRAMU YA KIKUNDI MLEZI KWA WANAWAKE WAJASILIAMALI

 Naibu Waziri wa Afya Maqendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili katika Ofisi za Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe alipofanya ziara ya siku moja ya kuamsaha ari ya wananchi kufanya shughuli za maendeleo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na vikundi vya wanawake wajasiliamali wa Wilaya ya Kisarawe na maeneo jirani wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kikundi Mlezi.
 Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga akieleza jinsi programu ya Kikundi Mlezi itakavyowasaidia wanawake kuleana na kusaidiana katika biashara zao ili kujikwamua kiuchumi wakati wa uzinduzi wa programu hiyo wilayani Kisarawe.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akikata utepe kuzindua rasmi Programu ya kikundi Mlezi itakayowezesha wanawake kusaidiana na kuleana wenyewe kwa wenyewe katika kuanzisha biashara ili kujikwamua kiuchumi.
  Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akionesha kibao kinachoonesha kuzinduliwa rasmi Programu ya kikundi Mlezi itakayowezesha wanawake kusaidia na kuleana  wenyewe kwa wenyewe katika kuanzisha biashara ili kujikwamua kiuchumi.

 Baadhi ya wanawake wa Wilaya ya Kisarawe wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa uzinduzi wa Programu ya Kikundi Mlezi iliyofanywa na Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile Wilayani Kisarawe Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akimkabidhi zawadi ya shuka Afisa Maendeleo ya Jamii Wilaya ya Kisarawe Bi. Mary Isala ikiwa ni zawadi kutoka kwa Kikundi cha wanawake cha Tutashinda  kilichopo Wilayani hapo kwa kudhamini jitihada na mchango wa Afisa Maendeleo ya Jamii huyo.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akingalia moja ya bidhaa zinazotengenezwa na kikundi cha wanawake wajasiliamali  cha Tutashinda Wilayani Kisarawe wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile akinunua mvinyo kwa moja ya kikundi cha wanawake wajasiliamali Wilayani Kisarawe ikiwa ni kuunga mkono uzaendo wa  kununua bidhaa kutoka kwa wazawa wakati alipofanya ziara ya kikazi Mkoani Pwani.
 Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa Wizara, viongozi wa Mkoa wa Pwani, Wilaya ya Kisarawe na wanawake wajasiliamali kutoka Wilaya ya Kisarawe mara baada ya kumaliza ziara yake ya kikazi mkoani hapo. Picha zote na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW

Na Kitengo cha Mawasiliano WAMJW
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amezindua programu ya Kikundi Mlezi yenye lengo la kuwawezesha wanawake wajasilimali  wasio katika Sekta rasmi kuleana wenyewe katika kuanzisha na kuendeleza mitaji na biashara zao.

Dkt. Ndugulile amezindua programu hiyo wakati alipofanya ziara Wilayani Kisarawe mkoani Pwani katika zoezi la kuamsha ari ya wananchi kujishughulisha katika shughuli za maendeleo katika maeneo yao.

Dkt.Ndugulile amesema kuwa  ili kufanikisha kufikia Tanzania ya viwanda Serikali itaendelea kuwasaidia wajasiliamali wadogo wadogo hasa wanawake katika kuwawezesha kuanzisha vikundi vitakayoanzisha viwanda vidogo vidogo na vya kati.

Ameongeza kuwa lengo la kuzindua Programu ya Kikundi Mlezi ni inalenga kuwawezesha wanawake wasio katika Sekta rasmi kwa kuwashirikisha wanawake wajasilimali waliokomaa katika biashara kuwalea na kuwasaidia wanawake wajasiliamali wanaoanza shughuli hizo.

“Niseme programu hii itasaidia kwa asilimia kubwa kuibua wanawake ambao hawakuwa na uwezo katika kuanzisha biashara zao na kufanya wanawake kujiunga na vikundi kukuza biashara na miradi yao na hatimaye kuanzisha viwanda vidogo na vya kati”alisisitiza Mhe. Dkt. Ndugulile.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bibi.Sihaba Nkinga amesema kuwa programu ya Kikundi Mlezi itasaidia kuwainua wanawake na kujitokeza kwa wingi kujishughulisha na shughuli za uzalishaji.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kisarawe Bw. Musa Gama amesema kuwa ataendelea kushirikiana na Wizara kuhamasisha wanawake kujitokeza na kujiunga na vikundi na kusaidiana katika kuendesha biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Mmoja wa wanawake wajasiliamali Wilayani Kisarawe Bi. Lydia Jacob ameishukuru Serikali kwa kuzindua Mpango huo utakaowawezesha wanawake kuleana na kusaidiana  katika kuanzisha na kuinuka katika biashara ambazo zitawasaidia kujikwamua kiuchumi.

Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile amefanya ziara ya siku moja mkoani Pwani na kuwatembelea wanawake wajasiliamali katika kuhamasisha wanawake kujishughulisha ili kusaidia kufikia azma ya Serikali ya Awamu ya Tano ya kuwa na Tanzania ya Viwanda.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad