HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 5, 2017

MBUNGE VITI MAALUM IRINGA ROSE TWEVE AIBUKA MSHINDI WA PILI MBIO ZA MITA 100 NA 200

 Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rose Tweve (kushoto)  ni Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko baada ya kumaliza mbio katika mashindano ya mabunge ya Jumuiya ya Afrika Mashariki kwa upande wa  Riadha yaliyoshirikisha wabunge kutoka Kenya na Uganda

Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Iringa Mhe Rose Tweve ameibeba timu ya riadha ya Wabunge wa Tanzania baada ya kuibuka mshindi wa pili wa mbio za mita 100 na 200.

Katika mbio zingine Josepha Komba mbunge wa viti Maalum Tanga aliibuka mshindi wa kwenye mbio za  mita 1500.

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Iringa Rose Tweve kazini sambamba na Mbunge Zubeda sakura.

Mashindano ya Wabunge ya nane kwa nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki yamezidi kuwa na sura mpya kila siku kwa timu zote kujiandaa ili waweze kuibuka na ushindi.

Rose amesema kuwa amefurahi kuweza kushika nafasi ya pili kwenye mbio za mitaa 100 na za mita 200 kwani anaamini mwaka unaofuata atafanya mazoezi kwa sana na kufanya vizuri zaidi.

Amesema kuwa  Mkoa wa Iringa ni miongoni mwa mkoa wenye wanamichezo tegemeo katika timu ya Bunge la Tanzania.

Takribani wabunge  nane wa mkoa wa Iringa wanashiriki kwenye michezo mbali mbali ambao ni Kocha wa timu ya soka ambaye pia mshiriki wa mchezo wa kutembea kwa kasi Walk-race Venance Mwamoto (Kilolo), Mahmoud Mgimwa ( riadha na kuvuta kamba), Menard Kigola (riadha/Kuvuta kamba),
Ritha Kabati (netball/volleyball),
Godfrey Mgimwa a.k.a Neymar (soka) ,Rose Tweve (Riadha), Cosato Chumi a.k.a Gazza (soka) na Mchungaji Peter Msigwa-kiungo mshambuliaji (soka)
Wabunge wakifurahi pamoja baada ya kumaliza mbio na wakipongezwa na wabunge wengine.
Mbunge wa Viti Maalum Iringa Rose Tweve akiwa katika pozi kabla ya kuanza kwa mbio.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad