HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 5, 2017

KAMATI YA UN KUTETEA HAKI ZA MSINGI ZA WAPALESTINA YAKUTANA NA BALOZI MAHIGA

Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (wa pili kulia) na wajumbe wengine wa kamati hiyo wakimkabidhi Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (wa kwanza kushoto) kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea.
Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour (katikati) akisaini kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli kabla ya kumkabidhi Balozi Augustino Maiga.

Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (katikati) akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya mazungumzo na Kamati maalumu ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina alipokutana nayo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour

Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) mara baada ya mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga (kulia) akipitia kitabu cha historia na taarifa mbalimbali za mwenendo wa majadiliano kutafuta suluhu ya mgogoro wa Wapalestina na Waisraeli walipo mtembelea mara baada ya kukabidhiwa.Kutoka kushoto ni Balozi wa Palestina katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Dk. Riyad Mansour na Balozi wa Senegal katika Umoja wa Mataifa (UN) na mjumbe wa Kamati ya UN kutetea haki za msingi za Wapalestina, Mr. Fode Seck.
Sehemu ya wajumbe wa Kamati ya Umoja wa Mataifa (UN) iliyoundwa kutetea haki za msingi za raia wa Wapalestina ikiwa katika mazungumzo na Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa, Balozi Augustino Maiga.
Ofisa Habari wa Kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Stella Vuzo akitoa utaratibu wa mazungumzo katika mkutano huo na wanahabari.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad