HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 19, 2017

JKT RUVU KUTUMIA MCHEZO WA FA KUTOA HESHIMA ZA MWISHO KWA WANAJESHI 14


Kikosi cha timu ya JKT Ruvu kesho kinatarajia  kushuka dimbani kumenyana na timu ya Mvuvumwa FC katika mchezo wa kombe la FA unaotarajiwa kupigwa kwenye uwanja wa Azam Complex kuanzia saa moja usiku.

JKT Ruvu inayoshiriki ligi daraja la kwanza wanakutana na Mvuvumwa kwa ajili ya kusaka nafasi ya kuingia nafasi inayofuata ya michuano ya Azam Sports HD inayojulikana kama FA huku wakiratajia kutumia mchezo huo kwa ajili ya kuwakumbuka na kutoa heshima ya mwisho kwa askari wa JWTZ waliofariki wakiwa kwenye majukumu ya kikazi nchini Demokrasia ya Congo.


Afisa Habari wa timu ya JKT Ruvu,Costantine Masanja alisema kwamba kikosi cha timu hiyo ambacho kinaongozwa na kocha Bakari Shime kipo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambao anaamini utakuwa na ushindani wa hali juu.


Alisema kwamba timu ya JKT Ruvu katika mchezo huo itafunga vitambaa vyeusi na kusimama kwa dakika moja kabla ya mchezo ikiwa ni kumbukumbu na heshima kwa askari wa JWTZ 14 waliokufa nchini Congo katika jukumu la ulinzi wa Amani chini ya umoja wa mataifa.

JKT Ruvu iliyochini ya Jeshi la Wananchi imejipanga kuhakikisha inarejea ligi kuu msimu ujao wakiwa wamejizatiti ambapo mpaka sasa wameshajinyakulia alama 25 wakiongoza kundi A wakifuatiwa na African Lyon wenye alama 17 na mpinzani wake katika mchezo wa FA Mvuvumwa akiwa anashikilia mkian kwa alama 4.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad