HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 19, 2017

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI JUU YA KUAHIRISHA KIKAO CHA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA

 Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa inavitangazia Vyama vya Siasa na umma kwa ujumla kuwa kikao na Semina ya Baraza la Vyama vya Siasa vilivyokuwa vifanyike siku ya tarehe 21 na 22 Disemba 2017, Jijini Dar es Salaam vimeahirishwa hadi hapo tarehe nyingine itakapopangwa.

Kikao hicho kimeahirishwa kwa ajili ya kutoa fursa kwa Vyama vya Siasa na wadau wa Vyama vya Siasa kushiriki katika shughuli za uchaguzi mdogo unaotarajiwa kufanyika 13 Januari 2018.  Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza kutokana na mabadiliko hayo. 
Jacqueline Kilama
Kny: MSAJILI WA VYAMA VYA SIASA
19 Disemba, 2017

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad