HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, December 19, 2017

MKURUGENZI MTENDAJI WA DCB AAGA RASMI, AMTAMBULISHA MKURUENZI ANAYECHUKUA NAFASI YAKE

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa akizungumza na waandishi wa habari na kuwaaga rasmi kna nafasi yake kuchukuliwa na Godfrey Ndalahwa leo Jijini Dar es Salaam.


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
MKURUNGEZI Mtendaji wa Benki ya DCB Edmund Mkwawa ameaga rasmi wanahabari pamoja na wateja wa benki hiyo baada ya kuwa kwenye kiti hicho kwa miaka 16 sambamba na kumuachia kijiti mkurungenzi mpya anayekuja kuchukua nafasi yake.


Mkwawa amemkaribisha rasmi Mkurugenzi Mtendaji anayetarajia kukalia kiti chake Godfrey Ndalahwa wakati wa mkutano wake na wanahabari leo Jijini Dar es Salaam.


Akizungumza baada ya utambulisho, Mkwawa amesema kuwa kwa kipindi cha miaka 16 benki  ya DCB iliweza kufanya vizuri na katika kipind cha miaka mitatu mfululizo wameweza kuanzia 2012 hadi 2014 wameshika nafasi ya tatu miongoni mwa benki zote kiujumla kwa ubora wa uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu ya kibenki.

Mbali na tuzo hiyo, pia wameweza kushinda na kushika nafasi ya kwanza katika mashindano ya uandaaji na uwasilishaji wa taarifa za mahesabu ya benki kwa mwaka 2016 kwa sekta za benki ndogo na za kati kwa ubora ikiwa ni kwa mwaka wa pili mfululizo kuanzia 2015 ambapo tuzo hizo huandaliwa na Bodi ya Taifa ya wahasibu na wakaguzi wa mahesabu NBAA.


Godfrey Ndalahwa nayetarajia kuchukua nafasi Mkurugenzi Mtendaji, amesema kuwa Benki imejipanga kuendeleza malengo yake na kuhakikisha inakuwa chaguo la kwanza la wateja katika utoaji huduma za kifedha. Katika kutimiza malengo haya, benki itatumia teknolojia ya kisasa katika utoaji wa huduma zake kupitia huduma ya DCB Pesa (kupitia simu ya mkononi) na DCB Jirani (Huduma kupitia wakala) kwa lengo la kuwafikia wateja wengi walengwa ambao ni wajasiriamali wadogo na wa kati waliosambaa kote nchini hadi vijijini.


Mojawapo ya malengo ya benki kwa mwaka unaokuja wa 2018 ni kuhakikisha inaongeza wigo na viwango vya utoaji huduma na kuwafikia wateja wengi zaidi wanaohitaji huduma za kibenki ikiwemo wamiliki wa Vikoba na Wafanyabiashara wa kati ambao wamehitimu hatua za mikopo ya awali katika benki hii. Hii ni kuhakikisha benki inakua pamoja na wateja wake na haitowaacha kuwahudumia katika mahitaji yao hata wakiongeza wigo wa biashara zao.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad