HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 27, 2017

WASHINDI WA DROO YA TATU WA PROMOSHENI YA ZALI LA MWANASPOTI WAKABIDHIWA ZAWADI ZAO

Kampuni ya Mwananchi Communications Limited(MCL), kupitia kampeni maalumu ya kazeti lake nguli la michezo la Mwanaspoti katika promosheni ya Zali la Mwanaspoti imekabidhi zawadi za washindi wa droo ya tatu wakati wa tamasha kubwa lililofanyika Viwanja vya Toto Tundu Tabata.

Zawadi zilizokabidhiwa ni pamoja na Tiketi ya kwenda kushuhudia Ligi Kuu ya Wingereza Ulaya ,Pikipiki moja, Tv 2, nchi 32, zikiwa na vingamuzi vyake vikiwa vimeunganishwa na kifurushi cha mwezi mzima pamoja na simu 2(Smartphone).
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kulia) akimkabidhi Gogfrey Mpiluka zawadi ya Simu ya mkononi(Smartphone) mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Salvatory Mtenga zawadi ya TV nchi 32, ikiwa na king’amuzi cha Azamu kikiwa kimelipiwa mwezi mzima mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Joyce Eosmsiles zawadi ya Simu ya mkononi(Smartphone) mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.
Afisa Masoko wa Kampuni ya Mwananchi Communications Limited, Huldermary Munisi(kushoto) akimkabidhi Fadhili Mahiche zawadi ya Pikipiki mara baada ya kuibuka msindi wa droo ya tatu ya Zali la Mwanaspoti inayoendelea nchini.Makabidhiano hayo yalifanyika katika katika tamasha lililofanyika Viwanja vya Toto tundu Tabata Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad