HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 15, 2017

NAMTUMBO KUANZISHA TAMASHA LA MUZIKI KUCHANGIA UJENZI WA KITUO CHA REDIO YA JAMII NAMTUMBO.

Halmashauri  ya Wilaya  ya Namtumbo  Mkoani Ruvuma  katika  harakati yake  ya  kuhakikisha  wanajenga  kituo  cha Redio  ya jamii katika  Halmashauri  hiyo  imepanga  kuanzisha  Tamasha  la  muziki  kwa lengo  la kupata  fedha  kujenga  kituo   cha Redio.
Kamati  ya uanzishwaji  Redio  katika  Hamashauri  hiyo  imependekeza  kuundwa kwa kamati  ndogo itakayoratibu  kuanzishwa  kwa Tamasha  la muziki  kwa  lengo  la kuchangia ujenzi  wa kituo hicho  cha Redio.
Aidha  mwenyekiti  wa  kamati ya uanzishwaji  Redio ya Halmashauri  ya Wilaya  ya Namtumbo  Bwana  Gwakisa  Mwasyeba  ambaye  ni   Afisa  mipango  wa Halmashauri hiyo  alipendekeza  majina  ya kamati  hiyo  kuwa ni  James komba  Afisa  utamaduni wa wilaya hiyo , Afisa  manunuzi  Robert  Mahili, Abbas  Masawe  katibu wa mikutano  ya madiwani , na Afisa  michezo  John  Ligoho na kuwataka kuanza  mikakati ya kuanzishwa kwa  Tamasha hilo la muziki.
Hata hivyo kamati ya  uanzishwaji  Redio  ya Halmashauri hiyo ilipendekeza  Hadidu  Rejea  kwa  kamati hiyo  ndogo  ili  zianze  kushughulika  nazo  na kutoa  taarifa  kamili  kwenye  kamati  kuu ya  uanzishaji  Redio .
Hadidu  rejea  ilizotoa  kamati  ya  uanzishaji  Redio  kwa  kamati  ndogo  ya  uanzishwaji  tamasha  la muziki   ni  pamoja  na  kamati  hiyo  ifuatilie  Gharama  za  kuwaleta  wasanii  mkoani Ruvuma  na aina  ya  wasanii  wanaokubalika kwa sasa  katika  jamii, wafuatilie  pia  upatikanaji  wa  muziki  na jukwaa  kwa ajili ya  wasanii,Muda  sahihi  wa kufanya  tamasha  na namna ya kufanya matangazo  kwa jamii ili  jamii ijitokeze kwa wingi  katika tamasha hilo pamoja  na kuwasilisha mapendekezo  ya  uwanja  wa  kutumia.
Aidha  mwenyekiti wa kamati  ndogo  ya Tamasha  aliiambia kamati  ya  uanzishwaji Redio  kuwa  kamati yake  itafanya ziara  mjini songea  nakufanya  mahojiano  na  waliobobea  na maswala ya matamasha  mjini  songea  pamoja  na wadau wengine wa  muziki  na  kutoa taarifa  katika kamati ya uanzishaji Redio  ya Halmashauri hiyo.
Halmashauri  ya  wilaya  ya  Namtumbo  inahitaji  kukusanya  shilingi  milioni 104 ili kukamilisha  zoezi  zima  la  uanzishwaji  wa  kituo  cha  Redio    ikiwa  ni gharama  za  uagizaji wa  vifaa , ,utengenezaji  wa  studio,gharama zinginezo kama  utengenezaji wa thamani za ofisi  kama meza,kabati  na viti vya ofisi ambapo kwa jumla yake  inafikia  kiasi cha shilingi milioni 104.
Pamoja na  mikakati  hiyo  Halmashauri ya  wilaya  ya Namtumbo   itawaomba  wadau  kuweza kushiriki  katika  tamasha hilo kwa  lengo la kuchangia  ujenzi  wa  kituo  hicho cha Redio ambacho  kitakuwa  ukombozi  mkubwa  katika  Halmashauri hiyo  na wilaya kwa  ujumla  wakati  utakapofika.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad