HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Thursday, 23 November 2017

Bondia Mtanzania kutetea ubingwa wa GBC dhidi ya bondia wa Afrika Kusini

 Bondia Mtanzania Ibrahim Class Mgendera, anatarajia kutetea ubingwa anaoushikilia wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka nchini Afrika Kusini

Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa ambalo limedhaminiwa na kampuni ya simu ya Vodacom PLC pamoja na kampuni ya Azam, litafanyika jijini Dar es Salaam Novemba 25 2017 kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam.

Mgendera anashikilia ubingwa wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight”ambao alioutwaa nchini Ujerumani tarehe 1 Julai, 2017 kwa kumpiga Jose Forero wa Panama. Bondia huyo atakuwa ni kibarua kigumu cha kutetea taji hilo mbelea ya KOOS SIPHO SIBIYA kutoka AFRIKA YA KUSINI

Akiongea na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi,Yusuph Singo alisema maandalizi ya pambano hili yalianza siku tarehe 5 August siku ya hafla ya kumpongeza bingwa huyo ambapo mgeni  alikuwa ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mh. Harrison Mwakyembe ambapo Uongozi wa  bondia hiyo ilimwelezea Waziri mwenye dhamana na michezo kwamba, mkanda huo unapaswa kutetewa katika kipindi cha miezi mitatu tangu alipoupata na tayari kulikuwa na ofa mezani za kuutetea mkanda huo kutoka katika nchi za Marekani, Ujerumani na Ufilipino.

“Mheshimiwa alisikiliza hoja hizo na kuweza kuzifanyia kazi kwa kuwatafuta wadhamini na wadau wa michezo nchini ili kuwezesha pambano la kutetea mkanda huo lifanyike hapa nyumbani kwa kuhamasisha mchezo wa ngumi za kulipwa pamoja na kuwapa burudani mashabiki wa mchezo huo hapa nchini,alisema Singo

Nikiwa kama mwenyekiti wa maandalizi ninapenda kutoa shukurani zetu za dhati kabisa kwaniaba ya mheshimiwa waziri kwa Wadhamini wakuu wa masumbwi haya AZAM pamoja na Vodacom Tanzania PLC,kamati ya pamoja ya kufanikisha pambano hilo ikijumuisha Baraza la Michezo la Taifa, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Menejimenti ya Joe’s Gym na Kamishei ya Ngumi za Kulipwa Tanzania.

Akizungumzia kuhusu udhamini wao, Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Matina Nkurlu alisema kampuni yao imeamua kutoa udhamini ikiwa kama ni sehemu yake katika kuendeleza na kukuza mchezo wa ngumi

“Vodacom imekuwa ikiendeleza na kudhamini  michezo mbali mbali hapa nchini ikiwamo soka ambapo sisi ndiyo wadhamini wakuu wa Ligi ya Tanzania bara(VPL). Udhamini wetu hauishi tu kwenye soka bali kwenye michezo mingine mingi tunapenda kutoa wito kwa watanzania kujitokeza kwa wingi na vilevile tutawawekea na bidhaa mbalimbali ukumbini hapo na watazipata kwa bei nafuu kabisa na pia tutatoa elimu kwao kuhusiana na kifurushi chetu kilichopo sokoni kwa sasa cha Pinduapindua,” alisema Nkurlu

Bondia atakayepambana na Mgendera anatarajia kuwasili nchini tarehe 22 Novemba, 2017. Pambano hilo  litanogeshwa na mapambano ya utangulizi ya kimataifa likiwakutanisha mabondia kutoka Tanzania na Malawi, mabondia wanawake pamoja na burudani ya muziki kutoka kwa wasanii nguli wa muziki wa kizazi kipya.

 Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC, Matina Nkurlu (kushoto)akiongea na Waandishi wa habari (hawapo pichani)  katika ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,  wakati  wa kuwatambulisha  Bondia Mtanzania Ibrahim  Mgendera(Katikati) anayetarajia kutetea ubingwa wake wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight dhidi ya bondia kutoka Afrika ya Kusini KOOS SIPHO SIBIYA(hayupo pichani)  Pambano hilo la kimataifa la ngumi za kulipwa  limedhaminiwa na Vodacom Tanzania na Azam TV na  litafanyika  jumamosi  kwenye uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam,Kulia ni Mkuzaji wa Vipaji  vya ngumi Tanzania, Joe Anea.
 ondia Mtanzania,Ibrahim Mgendera(Kushoto)atakaye utetea ubingwa wake wa mkanda wa dunia wa Baraza la Ngumi Duniani (Global Boxing Council – GBC) uzito wa “Lightweight” (kushoto) na bondia kutoka nchini Afrika Kusini,KOOS SIPHO SIBIYA wakitambulishwa na Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania PLC,Matina Nkurlu kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano na vyombo vya habari  uliofanyika katika Ukumbi wa Habari Maelezo jijini Dar es Salaam, pambano hilo  la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania,Azam TV litafanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Meneja Uhusiano wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu(kushoto)akishuhudia mabondia Ibrahim Mgendera kutoka Tanzania na kocha wake (wapili kushoto)na bondia kutoka nchini Afrika Kusini,KOOS SIPHO SIBIYA na kocha wake(wapili kulia)wakitambulishwa kwa waandishi wa habari(hawapo pichani)wakati wa mkutano na waandishi hao uliofanyika Habari Maelezo jijini Dar es Salaam,  pambano hilo  la kimataifa la ngumi za kulipwa limedhaminiwa na Vodacom Tanzania PLC, AzamTV litafanyika siku ya jumamosi katika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam,Katikati ni mwamuzi wa mpambano huo wa Kimataifa  kutoka nchini Ujerumani, Arno Pokrandt.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad