HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 8, 2017

Msimamo wa Askofu Niwemugizi Katiba Mpya Siyo wa Kanisa - Kadinali Pengo

Baada ya Askofu wa Kanisa Katoliki nchini kusikika akidai Katiba mpya ndio kipaumbele cha sasa kwa wananchi, Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam, Mwadhama Kadinali Polycarp Pengo amewataka waumini wa Kanisa hilo na Watanzania kwa kuyachukulia maoni hayo kuwa si msimamo wa Kanisa Katoliki. 

Akizungumza mwishoni mwa wiki hii, Kadinali Pengo amesema kuwa kauli iliyotolewa hivi karibuni na Askofu wa Jimbo la Rulenge, Ngara mkoani Kagera, Severine Niwemugizi ni maoni binanfsi na si msimamo wa Kanisa Katoliki nchini.

Mwadhama Kadinali Pengo amesisitiza hilo wakati akitoa ufafanuzi juu ya sintofahamu iliyojitokeza miongoni mwa Watanzania na waumini wa Kanisa hilo kutokana na kauli ya Askofu Niwemugizi.

“Napenda kutamka moja kwa moja kwamba huo sio msimamo wa kanisa na hauwezi kuwa msimao wa kanisa kwa sababu sisi tunataratibu zetu za kuishauri Serikali au kuzungumzia masuala ya jamii,” alisema.

Pengo amefafanua kuwa kutokana na nafasi ya Uaskofu aliyonayo Askofu Niwemugizi, kauli yake inaweza kutafsiriwa kuwa ndio msimamo wa Kanisa Katoliki au wa Jimbo la Rulenge, Ngara lakini kimsingi kauli ile imekosa vigezo vya kuichukulia kama msimamo wa Kanisa au Jimbo anakotoka.

Akizungumzia juu ya suala la katiba mpya ambalo baadhi ya wanaharakati na wanasiasa wanajaribu kuligeuza kuwa ajenda kuu kwa sasa, Kadinali Pengo alisema yeye binafsi kipaumbele chake ni kuona huduma za jamii kama zile elimu na afya zinaendelea kuboreshwa kwa kasi kama ambavyo Serikali ya Awamu ya Tano chini ya Dkt. Magufuli ilivyoanza kufanya.

“Mtu akiniambia priority (kipaumbele) ya Tanzania ni katiba mpya inabidi anithibitishie huo ukipaumbele maana siwezi kuona mtoto anakufa kwa njaa au kwa kukosa dawa eti kwa sababu ya katiba mpya. Kwangu mimi katiba ni kitu ambacho kije baadae, si cha haraka, Pengo"

“Wanasiasa wasiache watoto wetu wafe kwa njaa kisa malumbano ya katiba. Wasiache watoto wakose shule kwa sababu hela zote zimeishia kwenye malumbano juu ya katiba,” Kadinali Pengo amesisitiza.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad