HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Friday, 14 July 2017

Dr ARNOLD KASHEMBE KATIBU MKUU MPYA WA SIMBA


Kamati ya utendaji ya klabu ya Simba iiliyokutana jana jioni kwenye moja ya kumbi za mikutano za Hoteli ya Serena iliyopo hapa jijini Dar es salaam,imemteua Dr Arnold Kashembe kuwa katibu Mkuu mpya wa klabu. 

Msomi huyo mwenye shahada ya Uzamivu na aliyekuwa Mhadhiri kwenye vyuo mbalimbali barani Ulaya, uteuzi wake unaanza mara moja. 

Pia kamati hyo imepanga kufanya Mkutano wake mkuu wa kawaida tarehe 13-8-2017, huku pia ikitarajiwa kufanya Mkutano Mkuu utakaojadili mabadiliko ya katiba tarehe 20-8-2017.

Mikutano hyo imeitishwa kwa kuzingatia takwa la kikatiba la klabu,linalotaka notisi ya kuitishwa mikutano hiyo,ifanywe sio chini ya siku Thelathini kabla ya mikutano yenyewe. 

Klabu inatarajia kutoa taarifa zaidi juu ya maandalizi na taratibu za mikutano hiyo katika Siku chache zijazo na inaendelea kuwaomba Wanachama na Washabiki wake muendelee kuwa na utulivu,hususan kipindi hiki ambacho baadhi ya viongozi wetu wakiwa kwenye Shauri lao,liliopo Mahakamani.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad