HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 10, 2017

Mradi wa Hakuna Wasichoweza wazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike mkoani Lindi

Aliekuwa Mkuu wa wilaya ya lindi,Yahaya Nawanda(katikati)akikata utepe kuzindua mradi wa”Hakuna wasichoweza” unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kujistiri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation na kuendeshwa na T-Marc Tanzania mkoani humo,Wengine katika picha kutoka kushoto ni Aisha Mahadni mwanafunzi wa shule ya msingi stadium,Renatus Rwehikiza aliekuwa mkuu wa Vodacom Tanzania Foundation,Mkurugenzi wa T-Marc Tanzania,Diana Kisaka na Lalat Saidi.
Baadhi ya wanafunzi wa darasa la sita wa shule ya msingi Stadium mkoani Lindi wakifurahia baada ya kukabidhiwa vifaa vya kujistili pindi wakiwa kwenye hedhi na aliekuwa Mkuu wa wilaya hiyo,Yahaya Nawanda(hayupo pichani)baada ya kuzindua mradi wa ”Hakuna wasichoweza” mkoani humo unaowapatia elimu ya hedhi na vifaa vya kustiri wasichana ili wasikose kuhudhuria masomo yao mashuleni,Mradi huo unadhaminiwa na Vodacom Tanzania Foundation na kuendeshwa na T-Marc Tanzania.

Mradi wa “Hakuna Wasichoweza” unaoendeshwa kupitia taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation na kutekelezwa kwa  ushirikiano wa Shirika lisilo la Kiserikali la T-Marc katika mkoa wa Lindi unazidi kuleta faraja kwa watoto wa kike ambapo kwa mwaka huu wasichana wapato 2,000 tayari  wamenufaika nao. 
Mradi huu ni mwendelezo wa program ya  Hakuna Wasichoweza uliozinduliwa miaka ya nyuma-Mtwara, umewafikia wanafunzi na walimu 10,000 mashuleni kupatiwa elimu ya afya ya uzazi na huduma ya vifaa vya kujisitiri (pedi) wakati hedhi kwa watoto wa kike.
Akiongea na mtandao huu Meneja ruzuku na Mawasiliano wa Vodacom Tanzania Foundation,Sandra Oswald alisema tangu mradi huu uanze umekuwa na mafanikio makubwa kwa kufikia idadi kubwa ya walengwa wanaosoma katika shule mbalimbali mkoani Lindi ambapo wameweza kupatiwa elimu kuhusiana na mabadiliko ya miili yao katika mchakato wa makuzi na wamewezeshwa kwa kupatiwa taulo za hedhi.Alisema Oswald
Naye mmoja wa wanafunzi walionufaika na mradi huu, Riziki Athuman (14) ambaye ni mwanafunzi wa darasa la saba katika shule ya msingi ya Tandangongoro akiongea  kwa niaba ya wenzake kuwa “Hivi sasa wanaelewa kuhusina na suala zima la hedhi na jinsi ya kukabiliana nalo hususani kujiweka katika hali ya usafi na kutumia taulo za kisasa ambazo zinatuwezesha kuendelea na masomo tofauti na awali ambapo wasichana wenzangu wengi walishindwa kuhudhuria vipindi shuleni wanapokuwa kwenye hedhi kutokana na kutokuwepo na mazingira rafiki. Suala la hedhi lilikuwa halizungumziwi kabisa tofauti na sasa ambapo linajadiliwa na kutafutiwa suluhisho la kukabiliana na changamoto zake hususan kujenga vyoo na miundombinu ya maji mashuleni ya kuwasaidia watoto wa kike wanapokuwa kwenye hedhi”. Alisema Riziki.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad