HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 10, 2017

MBEYA CITY WAANZA SAFARI YA KUJA KUIVAA YANGA WIKIENDI HII



KIKOSI Mbeya City Fc , leo kimeanza safari kuelekea jijini Dar es Salaam tayari kwa mchezo wa ligi kuu ya soka Tanzania bara dhidi ya wenyeji Yanga uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Taifa mwishoni mwa wiki hii.

Afisa habari wa kikosi hicho  Dismas Ten amesema kuwa jumla ya nyota 18 na viongozi 10 watakuwa kwenye msafara huo kwa ajili ya kuhakikisha City inafanikiwa kuibuka na pointi tatu muhimu na kujiweka kwenye mazingira mazuri katika msimamo wa ligi.

Ligi iko kwenye hatua za mwisho, huu ni mchezo muhimu na matarajio yao ni  kushinda na kupata matokeo muhimu kwenye mchezo wa jumamosi, kwani wanafahamu Yanga ni timu nzuri na iko kwenye mbio za ubingwa lakini hilo haliwapi hofu kwa sababu wana  kikosi kizuri.


Ten amesema katika duru ya kwanza waliweza kupata matokeo mazuri na sasa wanakwenda Jijini Dar kuhitimisha dhamira yao ya kupata pointi sita msimu huu kutoka kwao


Akiendelea zaidi Ten alisema City imekuwa na wiki nne za kujindaa vizuri ili kuikubali Yanga kwa kufanya mazoezi mazito ikiwa ni pamoja na kucheza michezo zaidi ya mitano ya kirafiki ambayo imesaidia kuimarisha uwezo wa nyota wa kikosi kiuchezaji na kuwaongezea Morari ya kutaka kushinda kwenye uwanja wa Uhuru.

"Tumekuwa na wiki nne za kujindaa, hatukucheza mchezo wowote baada ya sare ya 1-1 na African Lyon kwenye uwanja wa Sokoine April 13,hivyo nguvu zetu zote tunaziweka siku ya jumamosi kwenye uwanja wa Taifa,".amesema Ten.

Miongoni mwa nyota waliopo kwenye msafara huo ni pamoja na Mrisho Ngassa,Hassan Mwasapile,Tumba Lui na Zahoro Pazzi



Kwa upande wake kocha mkuu Kinnah Phiri amesema hana wasiwasi na mchezo huo wa jumamosi kwa sababu anaifahamu vyema Yanga hasa baada ya kuifuatilia kwenye michezo kadhaa na tayari ameandaa mbinu za kuhakikisha vijana wake wanapata ushindi.

"Sina wasiwasi,wakati huu ambao sikuwa na mchezo wa ligi nilikuwa nawafuatilia, najua mbinu zao na nimewandaa vijana wangu vizuri ni wazi tutashinda tena dhidi yao kama ilivyokuwa kwenye mchezo wa duru ya kwanza".

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad