HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 April 2017

ZFA UNGUJA YAFANYA UCHAGUZI KUJAZA NAFASI ZILIZOACHWA WAZI

Wajumbe wa Mkutano Mkuu wa chama cha soka (ZFA) wilaya ya Magharibi A Unguja wamemchagua Haji   Issa Kidali kuwa Mjumbe wa ZFA Taifa kufuatia uchaguzi mdogo uliofanyika April 4 mwaka huu kujaza nafasi iliyoacha wazi na Mussa Suleiman Soraga aliefariki dunia Februari 24 mwaka huu.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika katika ofisi za ZFA Magharibi A, Mwenyekiti wa kamati ya uchaguzi huyo Othman Ali Hamad alimtangaza Kidali baada ya kupata kura 33 kati ya 43 zilizopigwa huku mpinzani wake Abdallah Bakari Abdallah akipata kura 10.

Uchaguzi huyo uliohudhuriwa na Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Mohammed Ali Hilal Tedy na make wa mbunge wa jimbo la Mfenesini Mziwanda Ibrahim Abdallah aliekua Mgeni rasmi, pia aliekuwa Katibu wa timu ya Umoja Mbuzini Abrahman Saleh Rajab alichaguliwa kuwa Katibu Msaidizi wa ZFA hiyo kwa kupata kura 26 dhidi ya 16 alizopata mpinzani wake Mwajuma Ali Kombo kati ya kura 42 zilizopigwa.

Akizungumza kabla na baada ya kukamilika kwa uchaguzi huyo Mziwanda aliwapongeza wajumbe wa mkutano huyo na wagombea kwa kufanya uchaguzi guru na wa haki na kuwataka washindi hao kuendeleza umoja na mashirikiano ili kuongeza kazi ya maendeleo ya soka wilayani humo.

Katibu Mkuu wa ZFA Taifa Tedy aliwaasa viongozi wa chama hicho kufanya kazi kwa pamoja ili maendeleo ya soma ndani na nje ya wilaya hiyo yapatikane kwa haraka na kuwapongeza wagombea walioshinda na walioshindwa kwa kuoneaha ukomavu wa michezo na kuahidi kuwapa ushirikiano washindi. 

Akifunga mkutano huo Mwenyekiti wa ZFA hiyo Kheri Adam Ali aliwakumbusha wajumbe wa mkutano huo umuhimu wa kuendelea mshikamano kati yao na kusahau mambo vote yanahusiana na uchaguzi humo ili kuendelea na ligi ya wilaya hiyo iliyopo katika hatua ya 12 bora.

Katika hatua nyengine Mgeni rasmi katika hafla hiyo Mziwanda Ibrahim Abdallah alitoa ahadi ya kuzipatia timu zilizofuzu kucheza hatua ya nne bora ya wilaya hiyo seti moja ya jezi kila moja ili kuziongezea ari na motisha wa kushiriki ligi hiyo ambayo mshindi wa kwanza na wa pili wataiwakilisha wilaya hiyo katika mashindano ya ngazi ya Taifa.

Uchaguzi humo umefanyika ili kuziba pengo lililoachwa na Soraga aliefariki kwa ajali ya barabarani na kujiuzulu kwa Bakari katika wadhifa aliokuwa akiushikilia kabla ya kuomba kuchaguliwa katika uchaguzi humo..

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad