HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 4 April 2017

DENI LA TFF, SERENGETI BOYS WAPIGWA CHINI WAKIELEKEA KWA MAKAMU WA RAIS.Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

MAMALAKA ya Mapato Tanzania (TRA) kupitia kampuni ya Yono, wamelikamata basi la timu ya Taifa linalomikiwa na Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini (TFF) ambalo kwa sasa linatumiwa na timu ya vijana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Boys. 

Gari hiyo imechukuliwa katika Hotel ya Urban Rose likiwa linawasubiri wachezaji wa Serengeti Boys liwapeleke kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Samia Sulu

Akizungumza na Michuzi Globu, Mkurugenzi Mtendaji wa Yono Scolastica Kevela amesema kuwa wamelikamata gari za Taifa Stars leo mchana na wataendelea kuzikamata mali zingine zinazomilikwa na Shirikisho hilo.

Mama Kevela amesema kuwa, maagizo ya kuzikamata mali za TFF ni maagizo kutoka mamlaka ya Mapato na wataendelea kuzishikilia mpaka pale watakapolipa deni hilo sugu wanalodaiwa.

"tumeendelea kuzishikilia mali za TFF mpaka pale watakapolipa deni lao sugu, takribani wiki tatu tulifunga ofisi zao na uwanja pae Karume na tutaendelea kuzitafuta mali zao popote zilipo,"amesema Kevela.

Deni la TFF linatokana na kodi za mishahara ya aliyewahi kuwa kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars, Marcio Maximo kwa takribani miaka minne tokea 2016 hadi 2010 pamoja na mechi ya Brazili na Taifa Stars mwaka 2010 ambapo kodi yake haikulipwa mpaka leo.Shirikisho la Mpira wa Miguu (TFF) wamethibitisha hilo na kusema kuwa Wakati Serengeti Boys wakielekea kwenda nyumbani kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan kupata naye chakula cha jioni kwa mwaliko wake, maofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), wamekamata basi wanalotumia na kuwashusha njiani. Viongozi wa Serengeti Boys wanatafuta basi jingine kuitikia mwaliko wa Mama Samia na huenda wakachelewa mwaliko kutegemea kupatikana kwa usafiri mwingine.

Katibu Mkuu wa Shirikisho hilo Selestine Mwesigwa amesema kwamba deni hilo si la kwao peke yao kwani Wizara na Hazina ndio walengwa wakuu na wanaoathirika ni wao TFF na wamejaribu kumtafuta Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari Utamaduni na Michezo, Profesa Ole Gabirel ili kukutana kutatua tatizo hilo, lakini kwa bahati mbaya hawajafanikiwa.

Timu ya achezaji wa Serengeti Boys wamealikwa nyumbani kwa Mama Samia kwenye hafla maalum ya kuagwa kabla ya safari ya Morocco kesho kwenda kuweka kambi ya mwezi mmoja kujiandaa na fainali za U-17 Afrika nchini Gabon Mei mwakani na inatarajiwa kuondoka kesho Saa 10: 45 jioni kwa ndege ya Emirates kwenda Morocco kupitia Dubai, ambako watalala siku moja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad