HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 3, 2017

SUMATRA yasitisha mgomo wa nchi nzima wa vyombo vya usafiri

 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe (katikati) akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani  (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.
 Makamu Mwenyekiti wa Wamiliki wa Mabasi ya Mikoani  (TABOA) Bw. Abdallah Mohamed (katikati) akifafanua jambo kwa waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akielezea hatua ya kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini, kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti Usafiri wa Nchi Kavu na Majini (SUMATRA) Bw. Gillard Ngewe na kushoto ni Mwenyekiti wa wamiliki wa Daladala mkoa wa Dar es Salaam (UWADAR) Bw. Kismat Jaffar.
Waandishi wa habari wakiwasikiliza viongozi wa vyama vya usafishaji nchini wakati wakielezea hatua ya kusitishwa kwa mgomo uliopangwa kufanywa na wasafirishaji wa abiria na mizigo nchini mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Picha na Eliphace Marwa – Maelezo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad