HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Monday, 3 April 2017

WENYE USONJI ILI WAPEWE SHUGHULI MBALIMBALI ZA KIJAMII ZITAKAZO WAFANYA WASIJIONE WAPWEKE - DKT. GHARIB BILAL

Makamu wa Rais Mstaafu, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (watatu kutoka kulia) akiongoza matembenzi katika siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir leo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal amewataka wadau mbalimbali kuwapa fursa watoto wenye usonji ili waweze kushiriki kwenye shughuli mbalimbali za kijamii zitakazo wafanya wasijione wapweke.

Dkt. Bilal ameyasema hayo mwishoni mwa wiki jijini Dar es Salaam katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir. ambapo ameipongeza taasisi hiyo kwa kuanzisha kitengo maalum kinachotoa mafunzo kwa watoto wenye usonji na kufafanua kuwa siyo kazi rahisi kwani inahitaji rasilimali watu, wataalamu, fedha kuwa na moyo na uthubutu hivyo wadau na serikali kwa pamoja waunge mkono jitihada hizo na atafikisha kilio hicho kwa serikali ili kuunga mkono jinsi ya kuwasaidia watoto hao.

Dkt. Bilal amesema kila umri unavyozidi kwenda ndiyo kiungo kimoja baada ya kingine vinavyopoteza mawasiliano na hatimaye kupatwa na usonji ni vyema kujitoa kwa hali na mali  kuwafanya nao wawe ni  sehemu ya jamii, kwani malipo yake yanatoka kwa Mungu.

Dkt. Bilal amechangia kiasi cha shilingi milioni moja huku akiahidi kuwa Makamu wa Rais Samia  Suluhu Hassan atachangia milioni 5 katika jitihada za kuwasaidia watu wenye usonji.

Kwa upande wake Bwana Imtiaz Lalji ambaye ni mwenyekiti wa bodi ya KSIJ ameeleza kuwa jamii ndiyo inabidi iwe rafiki wa karibu wa watu hawa na kutimiza ndoto zao za kimaisha, huku akieleza kuwa kwa upande wao KSIJ wametoa ajira za wanafunzi watatu kwa watu wenye usonji kama walimu wasaidizi na kutoa wito  kwa serikali na sekta binafsi kutoa nafasi za ajira kwa watu wa namna hiyo.
                       
Maadhimisho hayo ya siku ya usonji duniani yamebeba kauli mbiu isemayo "Tuwalinde na Tuwapende".
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (alievaa kofika) akikata utepe kufungua matembezi siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir leo jijini Dar es Salaam.
Matembezi yakiendelea.
Makamu wa Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal akisoma hotuba yeke katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir leo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa bodi ya KSIJ,Imtiaz Lalji akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni Rasmi,Makamu wa Rais Mstaafu,Dkt. Mohammed Gharib Bilal ili aweze kuzungumza na Wadau mbali mbali walioshiriki katika kuadhimisha siku ya usonji duniani iliyoandaliwa na taasisi ya 'KSIJ Central Board of Education' katika shule ya Al-Muntazir leo jijini Dar es Salaam.picha zote na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad