HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 March 2017

AGGREY MORRIS AREJEA UWANJANI, AANZA MAZOEZI MEPESI


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

BEKI kisiki wa Klabu Bingwa ya Afrika Mashariki na Kati Azam FC, Aggrey Morris ameanza rasmi mazoezi mepesi ya uwanjani baada ya kupata nafuu ya majeraha yake ya mfupa wa paja la kulia.


Morris alipata majeraha hayo wakati Azam FC ikiichapa Mbabane Swallows bao 1-0 katika mchezo wa kwanza wa Kombe la Shirikisho Afrika, ambapo katikati ya wiki iliyopita alianza na programu ya mazoezi ya ‘gym’ kabla ya leo kuhamia uwanjani.

Beki huyo anarejea wakati Azam FC ikiwa kwenye maandalizi ya mchezo ujao wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara (VPL) dhidi ya Yanga, utakaofanyika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam Jumamosi ijayo saa 10.00 jioni.

Akizungumza Morris alionyesha furaha yake huku akiomba sapoti kwa mashabiki, viongozi na wachezaji wenzake. “Namshukuru Mungu kwa kuweza kurejea uwanjani kwa sababu mchezaji lengo lake ni kucheza na sio kukaa juu (jukwaani), hamna kitu kibaya kwa mchezaji kama majeraha yakikuandama mara kwa mara yanaweza kukupotezea akili yako yote ya mpira,” alisema.


Morris akizungumzia mchezo ujao dhidi ya Yanga na kusema yupo vizuri kwa ajili ya mchezo huo huku akidai kuwa wamejipanga kushinda mtanange huo. “Kusema kweli mchezo ni mgumu kwa sababu Yanga ukiangalia ni timu kubwa, naiheshimu, ina wachezaji wazuri imejiandaa kwa sababu ukiangalia wao wanataka ubingwa, ila na sisi tumejiandaa vizuri kuhakikisha tunawafunga kwa sababu lengo letu sisi ni kushinda kila mchezo unaokuja mbele yetu, tukiwa kama Azam tunauhitaji sana mchezo huu ili kuendeleza katika nafasi ya pili tunayoitarajia,” alisema.


No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad