HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 28 March 2017

WAANDISHI WA HABARI WATAKIWA KUUNDA CHAMA KITAKACHO TETEA MASLAHI YAO

 Katibu mkuu wa CHODAWU, Said Wamba akizungumza na waandishi wa habri juu ya warsha ya tafiti kwa wafanyakazi wasio katika sekta rasmi

 Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Wito umetolewa kwa waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari  nchini  kuunda chama chao cha Wafanyakazi ambacho kitaweza kutetea maslahi yao katika kazi.

Hayo yamezungumzwa na Katibu mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Sekta isiyokuwa rasmi (CHODAWU), Said Wamba alipokuwa akifungua Warsha juu ya tafiti kwa wafanyakazi hao Jijini Dar es Salaam

"Waandishi wa habari wamekuwa mstari wa mbele katika kutetea maslahi ya wafanyakazi wengi hapa nchini lakini cha kushangaza mpaka sasa hawana chama chao ambacho kinaweza kuwatetea pindi wanapopata matatizo na wanapohitaji kupanga maslahi yao" Amesema Wamba.

aidha ameongeza watu wengine ambao wamekuwa wakidhalaurika kuwa ni wafanyakazi wa ndani ambao wanachama chao ambacho kina watetea lakini wengi wao wamekuwa wazito kujiunga.

ametoa wito kwa wadau wote na watu ambao wanafanya kazi katika sekta isiyo rasmi kujiunga katika vyama vya wafanyakazi hili wawezekupata maslahi yao.
 Baadhi ya washiriki wa warsha hiyo wakifatilia kwa makini hotuba ya katibu mkuu wa CHODAWU.
Mratibu TUCTA Kanda ya Afrika, Vicky Kanyoka akizungumza na wadau mbalimbali ambao wameshiriki warsha hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad