HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 31 January 2017

TRA YATANGAZA MWISHO WA UHAKIKI KWA TIN NAMBA KWA MKOA WA DAR ES SALAAM


Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii 

MAMLAKA ya Mapato Nchini (TRA) imesema uhakiki wa namba ya utambulisho ya mlipa kodi ‘TIN Number’ kwa Mkoa wa Dar es Salaam  umekwisha na uhakiki mwingine utahamia Mikoa mingine. 

Akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi ,jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo amesema uhakiki TIN Number muda wake ulikuwa ukiongezeka kutokana na mahitaji. 

Kayombo amesema kuwa kwa sasa muda hautaongezwa ,na wenye Tin number hawatakiwi kutumia mpaka pele watakapopata maelezo katika ofisi za TRA ili waweze kuendelea kutumia namba hizo. 

Amesema uhakiki huo ulianza Agasti hadi Oktoba na kuongeza tena muda wa miezi mitatu ambao umeishia leo. 

Kayombo amesema kuwa wale ambao wana Tin number na zinadaiwa TRA wanazo na wanatakiwa kulipa kodi zao ambazo wanadaiwa. 

Amesema uhakiki wa Number unasaidia kupata taarifa za mfanyabiashara kwa namba ya simu, makazi, sehemu anayofanyia kazi pamoja na anuani za mlipa kodi. 

‘’Watu wote wenye Tin Number wasizitumie mpaka pele watapokuwa wamepata maelezo juu ya kuzitumia namba hizo za utambulisho wa wafanyabiashara’’ amesema Kayombo.

Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipa Kodi, Richard Kayombo akizungumza na Blogu ya Jamii ya Michuzi juu ya uhakiki wa Tin Namba leo jijini Dar es Salaam. 
 
Sehemu baadhi ya wananchi wakiwa katika uhakiki wa TIN namba leo jijini Dar es Salaam. (Picha na Emmanuel Massaka Globu ya Jamii).

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad