HABARI MPYA

Home Top AdPost Top Ad

Tuesday, 31 January 2017

Usajili Kili Marathon kufanyika Mlimani City jijini Dar

Usajili wa mbio maarufu za Kilimanjaro Marathon sasa utaanznia jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mlimani City, imefahamika.

Muandaaji mkuu na muanzilishi wa mbio hizo, John Addison alisema usajili huo utaania Mlimani City na hii itakuwa mara ya kwanza kwa zoezi hilo kufanyika jIjini Dar es Salaamtangu kuanzishwa kwa mbio hizo miaka 15 iliyopita.  

Alisema usajili huo utafayika Februari 18 na 19 eneo la kuegesha magari mbele ya mgahawa wa Grano pembeni ya KFC kuanzia saa nane mchana hado saa mbili usiku. “Tunaamini watu wengi watajitokeza kwa sababu itakuwa mwishoni mwa wiki,” alisema na kuongeza kuwa hii itapunguza msongamano wa usajili Mjini Moshi.
Meneja Mkuu wa Mlimani City, Pastors Mrosso alisema wanajivunia kuwa wabia wa Kilimanjaro Marathon ambazo kwao ni mbio kubwa na wanaamini watu wengi watajitokeza kujisajili na pia kutembelea maduka mbalimbali na kupata huduma kutoka Mlimani City.

Meneja wa Bia ya Kilimanjaro Premium Lager, Pamela Kikuli ambaye ni mdhamini mkuu aliwapongeza waandaaji kwa kuanzisha usajili wa Dar es Salaam na kusema itarahisisha zoezi zima na kuhakikisha kila mtu anasajiliwa kwa wakati na kuepusha msongamano wa watu siku za mwisho.

Umie Naye Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Kaskazini, George Lugata aliwataka washiriki wote watumie fursa hii vizuri ili waweze kushiriki katika mbio hizi.
Kwa mujibu wa Bw. Addison, Usajili Arusha utafanyika Kibo Palace Hotel Februari 21 na 22 kuanzia saa nane mchana hadi saa mbili usikuna Moshi usajili utafanyika Keys Hotel  Februari 23 (saa sita mchana hadi saa kumi na moja jioni), Februari 24 (saa nne asubuhi hadi saa kumi jioni) na Februari 25 (saa tatu asubuhi hadi saa sita mchana).

“Tumeongeza siku za usajili kwa vituo vyote ili watu wengi zaidi watumie fursa hii na kuepusha msongamano wa watu Mjini Moshi tunawaomba washiriki wote watambue kuwa safari hii usajili utafungwa mapema kabisa kwani hakuna usajili utaendelea baada ya saa sita mchana Februari 25,” alisema Bw. Addison.
Wadhamini wa mbio za mwaka huu ni Kilimanjaro Premium Lager-42km, Tigo 21km, GAPCO 10 km-walemavu, Grand Malt-5km. Wengine ni KK Security, TPC Limited, FNB, Kibo Palace, Kilimanjaro Water, CMC Automobile, Rwandair, Keys Hotel and new sponsors Anglo Gold Ashanti na KNAUF Gypsum.

Mbio za mwaka huu zitafanyika Februari 26 katika viwanja vya Chuo Kikuu cha Ushirika Moshi kuanzia saa kumi na mbili asubuhi

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad