HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 23, 2017

MAMIA YA VIJANA WASHIRIKI KATIKA ZOEZI LA UCHANGIAJI DAMU LILILOENDESHWA NA SHIRIKA LA AFYA NA ELIMU YA TIBA TANZANIA (TAHMEF)

Shirika la Afya na elimu ya tiba Tanzania limefanikiwa kuendesha zoezi la uchangiaji damu kwa wagonjwa wenye selimundu (Sickle Cell) Siku ya Jumamosi Januari 21, 2017 katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa Mwananyamala.
Muanzilishi wa shirika la Afya na Elimu ya Tiba (TAHMEF), Juliana Busasi (kushoto) akiwa na Muanzilishi wa Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa selimindu Tanzania, Arafa Said (kati) na mmoja wa vijana waliochangia damu (kulia)
Zoezi hili limepewa ushirikiano mkubwa kutoka kwa vijana wakitanzania kutokana na idadi ya wachangiaji damu siku hiyo ambapo asilimia 95% ya wachangiaji damu ni vijana walio chini ya umri wa miaka 30 na asilimia 5% tu wakiwa juu ya miaka 30.

Mbali na uchangiaji damu vijana wengi walioshiriki wametumia vyema mitandao ya kijamii katika kuhamasisha watanzania kushiriki katika zoezi hili la uchangiaji damu.
Zoezi hili limelenga kuhusisha uchangiaji Damu kwa wagonjwa wa Selimundu na hivyo kuelimisha na kuchochea uelewa juu ya ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell) pia kuhimiza uboreshaji wa huduma za Afya Nchini kama inavyotajwa katika lengo la tatu katika malengo ya maendeleo endelevu duniani (Sustainable development Goals)

Zoezi zima liliandaliwa na kuendeshwa na Shirika la Afya na Elimu ya Tiba Tanzania (TAHMEF) kwa kushirikiana na Taasisi ya umoja wa wagonjwa wa Selimundu Tanzania, Vijana wa umoja wa mataifa (YUNA) na Lions Club ya Msasani Dar es salaam.

Shukrani Ziwafikie watanzania wote walioshiriki katika zoezi hili kwa njia mbalimbali ili kuokoa maisha ya watanzania wenzetu wenye uhitaji wa damu salama.

Zoezi hili linatarajiwa kuendelezwa tena kila baada ya miezi mitatu.
Kijana wa Umoja wa Mataifa (YUNA)  akichangia damu.
Lions Club Msasani wakikabidhi mahitaji ya zoezi la uchangiaji damu kwa wanachama wa TAHMEF.
Da Sauda Simba pia alikuwa ni mmoja waliochangia damu kwa wagonjwa wenye selimundu (Sickle Cell) Siku ya Jumamosi Januari 21, 2017
Prof. Julie Makani akichangia Damu katika zoezi hilo.
Vijana wakijiandikisha kwa ajili ya kuchangia damu.
Wasichana pia hawakukaa nyuma katika zoezi hili, Baadhi ya Vijana wa Kike wakisubiri  kuchangia damu.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad