HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, January 23, 2017

WAZIRI MWIJAGE AKAGUA MANDELEO YA AWALI UJENZI WA KIWANDA KIPYA CHA VIGAE, CHALINZE MKOANI PWANI

  Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amepongeza jitihada zinazofanywa na muwekezaji wa kampuni TwyFord Tanzania Cereramics,kwa ujenzi wa kiwanda cha kutengeneza vigae "Tiles" katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Waziri Mwijage, amesema hayo alipotembelea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo, litakalojengwa kiwanda hicho cha kutengeneza vigae "Tiles" kitakachotoa ajira kwa watanzania zaidi ya elfu mbili katika mfumo rasmi,na ajira elfu nne zisizo rasmi.

Waziri Mwijage aliongeza kuwa," bidhaa hizo pia zitauzwa katika nchi majirani kama Zambia,Malawi, DRC,Rwanda, Burundi,Uganda na Jamhuri ya watu wa Afrika Kati na kusafirishwa nje ya bara.

Kwa upande Mbunge wa Jimbo la Chalinze Ridhiwani Kikwete, alisema kuwa ujenzi  wa kiwanda hicho kipo katika hatua ya mwanzo ya Ujenzi na kinataraji kukamilika Mwezi wa Saba na kufunguliwa Rasmi mwezi wa Nane mwaka huu.

 Ridhiwani alisema kuwa kiwanda hicho kitasaidia kufungua mji wa Chalinze na kufanya mji wa viwanda na biashara na hivyo kufungua fursa za kiuchumi na kupanua mji huo,katika sekta ya viawanda inayosimamia vyema na serikali ya awamu ya tano.

 “ujenzi wa kiwanda hiki ni Alama Chanya ya jinsi serikali ya awamu ya Tano ilivyojidhatiti kufungua fursa za viwanda katika Nchi yetu.Wananchi wa Chalinze na Pwani wameaswa kuendelea kujipanga kwa viwanda na fursa nyingi zaidi.”alisema ridhiwani.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (wa pili kushoto) akiwa ameongozana na Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (wa tatu kushoto), Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kushoto) wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani. Waziri Mwijage ameridhishwa na maandalizi ya ujenzi wa kiwanda hicho na kumpongeza muwekezaji wake hasa kwa kasi wanayoenda nayo. Kwa mujimu wa Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics ambao ndio wamiliki wa kiwanda hicho, amesema kuwa ifikapo mwanzoni mwa mwezi septemba mwaka huu, kiwanda hicho kitakuwa kimekamilika na kitaanza kufanya kazi. Uwepo wa kiwanda hicho, utaweza kufungua fursa za ajira kwa vijana mbalimbali nchini.
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage (katikati) akizungumza jambo Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Jack Feng (kulia) wakati alipotembea eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.

Mkurugenzi Rasilimali Watu wa Kampuni ya TwyFord Tanzania Cereramics, Beda Tindwa akitoa maelezo kuhusu mradi huku Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete akisisitiza jambo mbele ya
Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage.



Mbunge wa Jimbo la Chalinze, Ridhiwani Kikwete (kulia) akimuonyesha kitu, Waziri wa Viwanda na Biashara, Charles Mwijage wakati walipokuwa wakitembea na kukagua maendeleo ya awali ya eneo litakalojengwa kiwanda kikubwa cha kutengeneza vigae "Tiles" lililopo katika Kijiji cha Pingo, Chalinze Mkoani Pwani.













No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad