HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 13, 2016

MOURINHO AANZA KAZI MAN UNITED, WAFANYA MAANDALIZI YA MSIMU WA LIGI KUU YA 'EPL'

Kocha mpya wa  Manchester United, Jose Mourihon kushoto.
 Kocha mpya wa  Manchester United, Jose Mourihon akisimamia mazoezi ya Timu hiyo ikiwa ni maandalizi kuelekea msimu Mpya wa ligi ya Uingereza.
Wachezaji wa timu ya Manchester United wakijinoa kwaajili ya maandalizi ya msimu mpya wa Ligi kuu ya Uingereza (EPL) katika viwanja vya Old Trafford jijini London nchini Uingereza.

MTANDAO wa Manchester United umeweka wazi picha za mwanzo za mazoezi chini ya kocha mpya Jose Mourinho,  huku wachezaji Henrikh Mkhitaryan na Eric Bailly walikuwa miongoni mwa wachezaji walioanza mazoezi na kikosi hicho  pamoja na beki  kinda mwenye umri wa miaka 18 Axel Tuanzebe ambaye yupo kwenye mikakati ya kocha huyo na Tyrell Warren (17) ambaye ni beki wa kulia.

Mourinho ameanza mazoezi na wachezaji 23 huku Ibrahimovic akiwa bado hajajiunga na kikosi hicho ila ameweka wzi msimamo wake kuwa Manchester siyo timu ya kubeza ni ya kipekee na kwa aina ya wachezaji vijana aliokuwa nao watakuja kuwa moto wa kuotea mbali baadae.

Mafunzo kikosi:
Makipa:
 Joel Pereira, Sam Johnstone, Dean Henderson

Watetezi:
 Antonio Valencia, Guillermo Varela, Timothy Fosu-Mensah, Eric Bailly, Phil Jones, Daley Blind, Axel Tuanzebe, Luke Shaw, Tyler Blackett

Viungo:
 Michael Carrick, Ander Herrera, Jesse Lingard, Juan Mata, Ashley Young

Washambuliaji:
 Henrikh Mkhitaryan, Memphis, James Wilson, Will Keane, Andreas Pereira, Adnan Januzaj.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad