HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 13, 2016

MTOTO AGUNDULIKA AKIWA AMEFUNGIWA NDANI NA WAZAZI WAKE KWA MIAKA 11 MKOANI MBEYA

Na Emanuel Madafa, Mbeya
Katika hali isiyokuwa ya kawaida kijana  mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili, amegundulika kufungiwa ndani  kwa zaidi ya miaka 11 na wazazi wake katika eneo la Mwambenja Kata ya Ilemi Jijini hapa.                                                                  
Kijana huyo, mwenye umri wa miaka 20, ambaye amejulikana kwa jina la Fredrick Emmanuel ametajwa kuwa amekuwa akiishi ndani bila ya kutolewa nje  hali iliyochangia kwa kiasi kikubwa kudhohofisha mwili wake .
Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Kata ya Ilemi jijini Mbeya   mwenye tatizo la ulemavu wa viungo na akili akiwa anaedaiwa kuwa amelala ndani kwa zaidi ya miaka 11 sasa kwa kile kinacho elezwa kuwa ni kufichwa ndani na wazazi wake ili kuondoa aibu ya familia .
Mahali anapolala  kijana Emanuel Fedrick (20)Mkazi wa Mwambeja Kata ya Ilemi jijini kwa zaidi ya Miaka 11 sasa kwa kile kinachoelezwa kuwa ni kuficha aibu ya familia.
Kijana Emanuel Fedrick (20)  mwenye tatizo la utindio wa ubongo akiwa amebebwa na shangazi yake Stella Mbuligwe baada ya kutoka nje na  kufanyiwa usafi wa mwili.
Kijana Emanuel Fedrick (20) Mkazi wa Mwambenja Ilemi jijini Mbeya ambaye anatatizo la akili na ulemavu wa viungo akipelekwa ndani na shangazi yake ,Stella Mbuligwe baada ya kufanyiwa usafi na kupatiwa chakula. Picha na Emmanuel Madafa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad