
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
KOCHA Mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo'Julio' amesema kuwa msimu huu wanatarajia kuja na kasi nyingine kwani wameamua kufanya marekebisho kwenye kikosi chao na wamepunguza idadi ya wachezaji na kwa maandalizi wanayoyafanya basi watakuwa Leciester City wa Tanzania na kufanya maajabu makubwa sana. Awali Mwadui ilikuwa na wachezaji takribani 33 na sasa wameamua kuwapunguza na kufikia hatua ya kufikisha wachezaji 24.
Julio amesema, kwa msimu huu wamejipanga zaidi kuwezwa kufanya vizuri na zaidi wameshazoea mikikimikiki ya ligi kwani katika msimu uliopita hawakuweza kufanya vizuri kutokana na ugeni wao kwenye mashindano hayo ila amewataka timu zote zikar chonjo kwani hawatategemea kuona watakachokipata.
"Timu yangu msimu huu itakua ni zaidi ya moto wa kuotea mbali kwani msimu uliopita hatukufanya vizuri kutokana na ugeni wetu ila kwa sasa wajipange sana na sisi ndio tutakuwa Leciester ya Tanzania yoyote akija mbele yetu ataambulia kipigo tu ,"amesema Julio.
Kocha huyo mwenye kariba ya kuongea sana, amesema kuwa mshambuliaji Paul Nonga aliyerejea kwenye kikoso hicho hana tatizo nae kwani wakati anaondoka aliondoka kwa adabu aliwaaga na.wakampa baraka zote kwani alikuwa anatafuta maisha na hata baada ya kushindwa na kuamua kurudi nyumbani wamempokea kwa mikono yote miwili.
Nonga msimu wa 2015/16 mzunguko wa pili alijiunga na Yanga kwa mkataba wa mwaka mmoja lakini ameshindwa kupata namba ya uhakika.kwenye kikosi cha mholanzi Hans Van De Pluijm na kuishia kusugua benchi na wakati mwingine kutokupangwa kabisa na kuamua kuachana na wanajangwani hao na kurudi Mwadui Fc.
No comments:
Post a Comment