HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, July 13, 2016

YANGA KAMILI KUWAVAA MEDEAMA.

KUELEKEA Mtanage wa kukata na Shoka kati ya Yanga dhidi ya Medeama ya Ghana ikiwa ni mchezo wa tatu wa kombe la shirikisho hatua ya makundi kikosi cha Yanga chini ya Mholanzi Hans Van De Pluijm akisaidiwa na Juma Mwambusi wamendelea kujifua Katika viwanja vya Boko jijini Dar es Salaam leo.

Yanga wamepoteza michezo yake miwili ya mwanzo na katika mchezo wa kwanza dhidi ya Mo bejaia ya nchini Algeria walipoteza kwa goli 1-0 wakiwa ugenini na mechi ya pili ni kwenye dimba la taifa dhidi ya TP mazembe.

Mshambuliaji wa kimataifa kutoka nchini Burundi Amisi Tambwe ameanza mazoezi binafis na kesho anatarajiwa kujumuka na wenzake baada ya maendeleo yake kuendelea vizuri.
Kikosi cha Timu ya Yanga wakijifua kwaajili ya kuingia dimbani Julai 16 mwaka huu katika uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad