HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 6, 2012

Hali si Shwari kwa Mdau Albert Makoye,anataraji kwenda india kwa matibabu zaidi

Mkurugenzi Mkuu wa Hoteli ya Giraffe Ocean View,Dkt. Charles Bekoni (kulia) akiwa na Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania,Bw. Albert Makoye ambaye anasumbuliwa na ugonjwa wa pingili za chini za uti wa mgongo kutokana na kutenguka alipokuwa akifanya mazoezi yake ya kawaida ya kila siku,wakati alipofika nyumbani kwake leo kumjulia hali.Bw. Makoye ambaye pia ni Mdau Mkuu wa Globu ya Jamii anataraji kwenda nchini India kwa Matibabu zaidi ya Maradhi hayo hivi karibuni.Globu ya Jamii inampa pole sana Mdau Albert Makoye kwa maradhi hayo yanayomsumbua na inamuombea aweze kupona haraka na kuendelea na majukumu yake kama hapo awali.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad