HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, January 6, 2012

mwili wa Marehemu Azizi Sheween wawasili nchini leo

Rais Jakaya Kikwete na Rais Mstaafu alhaj Ali Hassan Mwinyi na waombolezaji wakiswalia mwili wa Marehemu Azizi Sheween Afisa Ubalozi wa Tanzania huko Abu Dhabi, UAE,ambaye alifariki dunia mwisho wa mwezi uliopita na mwii wake umeletwa leo Janaury 6, 2012 kutoka huko, umeagwa rasmi na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho.
Rais Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu Ahaji Ai Hassan Mwinyi, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh Bernard Membe, Katibu Mkuu Kiongozi Mh Ombeni Sefue na waomboezaji kwenye msiba wa Marehemu Azizi Sheween Afisa Ubalozi wa Tanzania huko Abu Dhabi, UAE,ambaye alifariki dunia mwisho wa mwezi uliopita na mwii wake umeletwa leo January 6, 2012 kutoka huko, umeagwa rasmi na kusafirishwa kuelekea nyumbani kwake Moshi kwa mazishi yanayotarajiwa kufanyika kesho. PICHA NA IKULU

Ratiba ya Mazishi ya Marehemu Aziz S.M. Sheween


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa inatangaza ratiba ya msiba wa aliyekuwa Mkuu wa Utawala wa Ubalozi wa Tanzania Riyadh, Saudi Arabia na Afisa Mambo ya Nje Mkuu wa Wizara Bw. Aziz Sheween.  

Mwili wa Marehemu Aziz utawasili Dar es salaam leo tarehe 6/01/2012 Saa Saba Mchana na kupelekwa nyumbani kwake Mikocheni kwa ajili ya Dua na Kumsalia Marehemu.  

Baada ya Kumsalia Marehemu, msafara wa Mwili wa Marehemu Aziz utaelekea Viwanja vya Ndege vya Mwl. J.K. Nyerere kwa ajili ya safari ya kuelekea Moshi, Kilimanjaro kwa mazishi.  

Marehemu Aziz Sheween anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 7/01/2012 baada ya Sala ya Adhuhuri Moshi Mkoani Kilimanjaro. 

Kwa niaba ya Uongozi na Wafanyakazi wote wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Katibu Mkuu wa Wizara Bw. John Haule anatoa pole kwa familia, ndugu, jamaa, marafiki na wote walioguswa na msiba huo. 
 
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano ya Serikali,
Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa,
P.O. Box 9000
Dar Es Salaam
Tanzania

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad