Tembo wakiwa ndio wanyama wanaoonekana kwa wingi katika hifadhi yetu ya Mikumi kwani hata ukiwa unapita barabarani ni lazima utawaona tu.hapa wakijipatia chochote kitu ili na wao waongeze siku za kuishi.
Swala na wao ndio kama hivyo tena,huwezi maliza hifadhi hii ya Mikumi bila kuwaona tena wakiwa katika hali ya uwingi.
Mnyama wa Taifa,Twiga nao wapo wengi ila mimi nilibahatika kumuona mmoja tu wakati nakatiza mbuga hiyo.
Nyati nao ndio usiseme,yaani wako kibaoooo..... kweli nchi yetu imejaaliwa kwa vivutio vingi,yaani ushindwe wewe tu.
Ndio, tuna hifadhi nzuri zenye wanyama wengi na ni kivutio sana kwa watu/watalii. Ila huwa najiuliza ni vivutio kwa watalii tu ? na sio kwa WATANZANIA WENYEWE? Hivi mnajua kuna watanzania wangapi wanajua Twiga anaonekanaje au Tembo? Ahsante kwa kunikumbusha Mikumi ni juzi tu nimepita hapa hata picha nilizopiga sijapata muda kuweka kibarazani kwangu:-)
ReplyDelete