Mmoja wa wasanii Spider Man(Yombo Chaka) akisherehesha kwa kutembea juu ya kamba wakati wa tamasha la burudani la wazi lililoandaliwa na kampuni ya Vodacom Tanzania jana katika ufukwe wa bahari ya Coco jijini Da res salaam kwa lengo la kutoa zawadi za fedha na televisheni kwa washindi wa promosheni ya Mega inayoendeshwa na kampuni hiyo nchini. Jumla ya washindi kumi na sita kila mmoja alikabidhiwa shilingi milioni 11.
Meneja Mauzo Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Henry Tzamburakis (kulia),
akimkabidhi mshindi wa promosheni ya mega Televisheni aina ya Samsung
LCD Bw.Peter Masawe aliyejishindia kwenye promosheni hiyo ya Vodacom
inayomnedelea nchini kote. Zawadi kwa washindi mbalimbali wanaotokeoa
mikoa ya Pwani zilikabidhiwa jana katika hafla iliyoambatana na tamasha
la lawazi la burudani katika eneo la Ufukwe wa Coco jijini Dar es
salaam.
Mkuu wa Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Atilio Lupala mwenye suti nyeusi
akimpa hongera Bw. Peter Masawe ambae ni mmoja wa washindi wa promoheni
ya Mega aliyejishindia Televisheni aina ya Samsung LCD wakati wa hafla
ya utoaji wa zawadi kwa washindi mbalimbali iliyofanyika jana kwenye
ufukwe wa bahari ya Coco jijini Dar es salaam.
Baadhi ya washindi wa promosheni ya Mega inayoendeshwa na Vodacom
Tanzania nchi nzima wakiwa na Televisheni aina ya Samsung LCD
walizojishindia na kukabidhiwa jana katika hafla iliyoambatana na
tamasha la wazi la burudani katika ufukwe wa bahari ya Coco – Oysterbay
jijini Dar es salaam.
Meneja Mauzo wa Vodacom Tanzania Kanda ya Pwani Henry Tzamburakis kulia, akimkabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 11 mshindi wa Promosheni ya Mega Bw.Said Mbegu inayoendeshwa na Vodacom Tanzania nchini,Jumla ya washindi 16 kila mmoja walikabidhiwa hundi zao hapo jana,anaeshuhudia katikati ni Mkuu wa Vodacom Kanda ya Pwani Atilio Lupala.Hafla ya kmakabidhiniano ilifanyika jana katika ufukwe wa bahari ya Hindi jijini Dar es salaam.
No comments:
Post a Comment