HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2011

Vodacom yadhamini mashindano ya uvuvi yalivyofana huko Sinda kisiwani


  Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akimkabidhi zawadi  Alfred Charles kwa niaba ya timu yake baada ya kuibuka washindi wa kwanza kwa upande wa boti ya Mistress katika mashindano yaliyofanyika huko Sinda kisiwani mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzani
 Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania Bw. George Rwehumbiza (kulia) akitoa zawadi kwa mshindi wa uvuvi kwa upande wa watoto Kyle Balarin (15) aliyekuwa akitumia boti  ya Tarkakatika mashindano yaliyofanyika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, (katikati) ni Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club akishuhudia utoaji wa zawadi hizo.
  Wafanyakazi wa boti ya Mistress wakiwa wamebeba samaki zilizovuliwa katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi  yajulikanayo kama Latham Open yaliyoshirikisha nchi sita  na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.
 Mwanamuziki Mark Hart kutoka Afrika Kusini akitumbuiza katika mashindano ya uvuvi yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda mwishoni mwa wiki, mashindano hayo yaliyoshirikisha nchi sita yalidhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.

 Washindi wa  mashindano ya uvuvi ya Latham Open wakifurahia tuzo zao za ushindi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo yaliyokuwa yakifanyika Kisiwani Sinda mwishoni mwa wiki na kudhaminiwa na Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania.
 Commodore Spiras Manoloudis wa Yatch Club jijni Dar es Salaam (kushoto) akitoa neon la shukrani kwa wadhamini wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyofanyika katika kisiwa cha Sinda hivi karibuni ambao ni Kampuni ya simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, (kulia) Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Bw. George Rwehumbiza.
 Kikundi cha Sanaa cha Jambo brothers kutoka Zanzibar kikionyesha sarakasi mbalimbali katika kisiwa cha Sinda wakati wa mashindano ya uvuvi (latham Open) yaliyokuwa yakiendelea kisiwani humo, ambayo pia  yalidhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mkononi ya Vodacom Tanzania.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad