Mkuu wa Wilaya ya Nzega, Florence Horombe, akipokea risala iliyosomwa na wanafunzi wa shule ya msingi, Nyasa 1 wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa vitabu vya kiada vyenye thamani ya zaidi ya sh. Milioni 5 vilivyotolewa na kampuni ya tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) hafla hiyo ilifanyika hivi karibuni shuleni hapo.
Wanafunzia wa shule ya msingi, Nyasa 1 iliyopo wilayani Nzega wakisoma vitabu vya kiada walivyokabidhiwa na kampuni ya tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) katika hafla iliyofanyika shuleni hapo hivi karibuni. Kulia ni Ofisa Ugawaji Rasilimali wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA), Anne Mlimuka.
Wanafunzi wa shule ya msingi Nyasa 1 iliyopo wilayani Nzega mkoani Tabora wakiimba kwaya wakati wa hafla ya makabidhiano ya vitabu vya kiada vilivyotolewa na kampuni ya tigo kwa kushirikiana na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa vitabu shuleni hapo.
No comments:
Post a Comment