HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, October 3, 2011

sugu wa enzi hizooooooo



Na John Kitime
Mwaka 1995, nikiwa najaribu kusambaza kazi za wanamuziki wa Tanzania kupitia kajimradi kadogo, mwanamuziki Innocent Nganyagwa alinijia na kunihadithia kuhusu mwanamuziki mpya wa Rap ambaye alikuwa tofauti na wasanii wenzie, kimawazo na hata jinsi ya sanaa yake ilivyo, na ndipo nikakutana na kusikia kazi ya MR2. 
Muziki wake ulinifurahisha kwa sababu mbili ya kwanza alikuwa akitumia Kiswahili kilichoeleweka tofauti na wasanii wengi wa Rap wa wakati huo ambao walighani Kiswahili utadhani wameshuka leo toka Marikani, pili alikuwa na ujumbe mzito, ambao hata leo miaka zaidi ya 15 toka ulipotolewa bado una maana kwa jamii ya Tanzania. 
Sishangai kuwa yeye sasa ni Mheshimiwa Mbunge Joseph Mbilinyi. Lazima nijisifu kuwa sikukosea kuanza kusambaza kazi yake ya kwanza album ya NI MIMI. Angalia video hii kwa makini utakuta mengi aliyosema atatimiza alitimiza.
Tembelea pia

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad