Baadhi ya wazee toka mikoa mbalimbali nchini wakiandamana wakiwa wamebeba mabango yenye ujumbe tofauti kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa yaliyofanyika mkoani Lindi hivi karibuni.
Timu ya wanawake kwenye mashindano ya mbio za magunia katika kilele cha maadhimisho hayo.
Licha ya changamoto zinazowakabili wazee,timu ya wanaume nayo hawakuwa nyuma katika mbio za kukimbia na magunia.
Wazee wameipongeza serikali katika miaka 50 ya uhuru kuwatambua kama rasilimali na hazina kubwa kutokana na uamuzi wake wa kutunga Sera ya Taifa ya Wazee ya mwaka 2003 pamoja na tamko lake la kutoa matibabu bila malipo katika hospitali zote za Serikali.Pichani ni timu mojawapo ya wazee toka mikoa mbalimbali wakivuta kamba kwenye kilele cha maadhimisho ya siku ya wazee duniani kitaifa mkoani Lindi.
Timu ya wanaume nao hawakuwa nyuma kwenye mashindano ya kuvuta kamba.Wazee hao wameiomba Serikali iwaingize kwenye mifumo ya mifuko ya afya kwa kuchangiwa na halmashauri zao.Picha zote na Catherine Sungura-Mohsw.
No comments:
Post a Comment