
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akizindua ramani inayoonyesha mtandao wa vituo vya matibabu vya ngazi mbalimbali na sehemu vilipo hapa nchini mara baada ya kutembelea Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo jijini Dar es salaam.Kulia ni Mganga Mkuu wa serikali Dkt Deo Mtasiwa na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba (aliyesimama nyuma ya Waziri)

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa akipata maelezo ya namna mtambo mkuu wa kuhifadhi kumbukumbu (main server)unavyofanya kazi ndani ya ofisi za Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya leo jijini Dar es salaam.

Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya Bw. Emanuel Humba(katikati) akimwonyesha Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Prof. David Mwakyusa maeneo mbalimbali na namna Mfuko huo unavyoendelea kuboresha miundombinu na kuweka mazingira mazuri ya utendaji kazi ili kuinua utoaji wa huduma kwa wateja.Picha na Aron Msigwa - MAELEZO.
No comments:
Post a Comment