SIKU YA WANAWAKE NA USIKU WA MWANAMKE (LADIE NIGHT) LA PRIMA JUMAMOSI.
KATIKA KUADHIMISHA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI/NCHINI TANAZANIA. KINA MAMA WENGI WAKIWA WAMEJIPANGA VYA KUTOSHA KUISHEREHEKEA SIKUKUU YAO AMBAYO IMEPANGWA KUFANYIKA KITAIFA HUKO MKOANI TABARA JUMATATU TAREHE 08/03/2010
WANAWAKE WOTE WAKIWEMO WAJASIRIAMALI WA MKOA WA DAR ES SALAAM, WANAAZA KUISHEREHEKEA SIKU HIYO, JUMAMOSI HII TAREHE 06/03/2010 NDANI UKUMBI WA LA PRIMA KATIKA USIKU WA MWANAMKE “LADIES NIGHT” HUKU KILA MMOJA AKIWA NA MWENZA WAKE HATA MPENZI WAKE.
KINA MAMA HAO WATASHEREHEKEA SIKUKUU YAO HIYO KWA KUJICHANA NYAMA CHOMA NA VINYWAJI VYA KUMWAGA HUKU RUMBA LA KIUTU UZIMA LIKISAKATWA KWA STAHA YA HALI YA JUU, LIKIONGOZWA NA MKONGWE KING KIKII PAMOJA NA WAZEE SUGU,UTAWEZA KUKIPEPERUSHA KITAMBAA CHEUPE NA WAZEE SUGU KWA SHILINGI 5,000/- TU.
HIVYO KINA MAMA WOTE MNATAKIWA KUFIKA BILA KUKOSA SIKU HIYO HUKU MKIWA MMEONGOZANA NA KINA BABA (WAUME /WAPENZI WENU) KATIKA UKUMBI WA LA PRIMA JUMAMOSI HII TUANZE KUSHEREHEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.
No comments:
Post a Comment