HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, September 27, 2009

Faida Ya Kuchat Wakati Unaendesha

hii ndio faida ya kuchat kwa simu huku ukijua unaendesha chombo cha moto,mwenye hiyo gari ndogo hapo aina ya Hiace super custome,alikuwa akiendesha gari lake kwa mwendo wa kasi kidogo na katika barabara ya Morogoro rodi na nilianza kumuona akiyumba yumba kimtindo lodini,ghafla nikaona kitu kimekwea baraza la katikati ya barabara halafu kikarudi tena lodini na kugeukia kilikotokea.tena anabahati sana huyu jamaa maana hilo daladala ndilo lililokuwa linamfuata kwa nyuma seme lilikuwa mbali kidogo ila kama lingekuwa karibu basi tungesikia mengine leo.hii ngoma iletokea mchana huu pale magomeni jirani kabisa na ile baa ya Highway a.k.a kwa Macheni. wasamalia kama kawa.

1 comment:

  1. Mzee wa mtaa ninaomba unipe tafsri ya neno LODINI kidogo sijafahamu hapo

    ReplyDelete

Post Bottom Ad