HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 27, 2009

Basi Mohamed Trans Lapata Ajali

baadhi ya watu wakiendelea kutoa miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali ya basi la Mohamed trans,iliyotokea majira ya saa kumi na mbili kasoro maeneo ya Korogwe mkoani Tanga,hadi sasa inasemekana idadi ya watu waliopoteza maisha katika ajari hiyo imefikia watu 28 huku wengine wakiwa hospitali wakiendelea kupata matibabu.MTAA KWA MTAA Blog inawapa pole ndugu,jamaa na marafiki wa marehemu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo,na mungu aziweke mahala pema peponi roho za ndugu zetu wote waliopoteza maisha kutokana na ajali hii.
-AMEEN

TAARIFA ILIYONIFIKIA HIVI PUNDE TOKA PANDE ZA KOROGWE MKOANI TANGA,ZINARIPOTI KUWA BASI LA MOHAMED TRANS LINALOFANYA SAFARI ZAKE KATI YA MWANZA-DAR,LIMEPATA AJALI MBAYA SANA MAENEO YA KOROGWE LIKIWA LIKITOKEA MWANZA KUJA DAR BAADA YA KUGONGANA LA LORI USO KWA USO NA KUSABABISHA VIFO VYA WATU KADHAA (IDADI BADO KUJULIKANA) NA WENGINE KUJERUHIWA VIBAYA SANA NA KUKIMBIZWA HOSPITALI,KWA MUJIBU YA MDAU ALIOPO MAENEO YA AJALI ANASEMA AJALI HIYO IMETOKEA MAJIRA YA SAA KUMI NA MBILI KASORO YA JIONI,AMBAPO YEYE ALIKUWA KWENYE GARI NYINGINE ILIYOKUWA NYUMA KWA UMBALI KADHAA NA BASI HIYO NA KUONA KILA KILICHOENDELEA KATIKA AJALI HIYO.TUTAENDELEA KUJUZANA NA KUPATA IDADI KAMILI YA NDUGU ZETU WALIOPOTEA KATIKA AJALI HIYO HAPO BAADAE KIDOGO.HIVYO TUVUTE SUBIRA KIDOGO.

1 comment:

  1. Ninasikitika kwa kupotea kwa ndugu zetu katika ajali mbaya kama hizo. Mungu azilaze mahala pema peponi roho za wote waliopoteza maisha yao. Polisi wa barabarani waache kupokea rushwa hawaoni kuwa roho zinazidi kuteketea???

    Othman ni AJALI bwana si ajari.

    ReplyDelete

Post Bottom Ad