HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, February 15, 2024

SPORTPESA YAJIVUNIA KUCHANGIA PATO LA TAIFA

 

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Sportpesa, Abbas Tarimba (wa kulia) akikabidhi mfano wa hundi ya kiasi cha Tsh. 265, 780, 681 kwa mshindi wa Supa Jackpot ya Sportpesa, David Mwenge, ambaye alibashiri michezo 13, hafla hiyo ya makabidhiano imefanyika jijini Dar es Salaam.


Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam
KAMPUNI ya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa inajivunia kuendelea kuchangia sehemu ya pato la taifa baada ya wateja wake kubashiri michezo mbalimbali na kushinda kiasi cha fedha ambacho kinachangia kodi ya taifa.

Akizungumza jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kukabidhi kiasi cha zaidi ya shilingi Milioni mbili (Tsh. 265, 780, 681) kwa mshindi wa Supa Jackpot, David Mwenge - Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Sportpesa, Abbas Tarimba amesema katika kiasi hicho cha fedha, Serikali imepata kodi yake asilimia 10.

Tarimba amesema Sportpesa imeendelea kuchangia fedha nyingi zaidi kila mwezi kupitia michezo hiyo ya kubashiri na kuendelea kuchangia ukuaji wa uchumi wa taifa la Tanzania. “Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wanasema sisi Sportpesa ni walipaji wakubwa wa kodi,” amesema Tarimba

Aidha, Tarimba amesema licha ya kuchangia kodi kwa taifa na ukuaji wa uchumi kwa ujumla, kupitia michezo hiyo ya kubashiri na baada ya washindi kupatikana, vijana wengi wameendelea kupata ajira, kuweka akiba benki na baadae kupata faida na kubadilisha maisha yao.

Kwa upande wake, Mkaguzi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini, Rasul Masoud amewapongeza Sportpesa kufika hatua hiyo ya kuwa walipaji wakubwa wa kodi kwa taifa, kukuza uchumi kupitia michezo hiyo ya kubashiri pamoja na kuinua hali za Watanzania wa kada mbalimbali.

Naye, Mshindi wa Supa Jackpot ya Sportpesa, David Mwenge amesema alianza kubashiri na Sportpesa tangu mwaka 2018 ambapo amekuwa akishinda kiasi cha fedha (Bonus) baada ya kubashiri michezo mbalimbali, Mwenge amesema hakupata usingizi alipopata ujumbe kuwa ameshinda kiasi cha fedha, Tsh. 265, 780, 681.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad