HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, February 17, 2024

Mamia Wajitokeza Dar Kuchukua Namba za Kili Marathon

 Mamia ya washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, leo walijitokeza katika viwanja vya Mlimani City kuchukua vifaa vya kukimbilia. Zoezi hilo litaendelea kesho Jumapili kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

MAMIA ya washiriki wa mbio za Kilimanjaro Premium Lager International Marathon zinazotarajiwa kufanyika Jumapili ijayo, leo walijitokeza katika viwanja vya Mlimani City kuchukua vifaa vya kukimbilia.

Kwa mujibu wa waandaaji wa mbio hizo, zoezi hilo litaendelea kesho Jumapili kuanzia saa sita mchana hadi saa kumi na mbili jioni.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Meneja Matukio wa mbio za Kilimanjaro Marathon, David Marealle alisema muitikio ni mkubwa.

"Watu wamejitokeza Kwa wingi kuchukua namba zao na ni matumaini yetu kuwa kesho ambayo ni siku ya mwisho Kwa Dar es Salaam washiriki watajitokeza zaidi," alisema.

Meneja huyo alisema Bado Kuna nafasi za mbio za Km 5 za Gee Soseji huku za Km 42 za Kilimanjaro Premium Lager na Km 21 za Tigo zimekwisha na usajili ulishafungwa.

Alitahadharisha kuhusu washiriki kukimbia na namba ambazo zimesajiliwa na watu wengine au namba za miaka ya nyuma.

Alisema baada ya Dar es Salaam zoezi hilo litahamia Arusha Februari 20 na 21 katika hoteli ya Kibo Palace na baadaye Moshi Februari 22,23 na 24.

Wadhamini wa mwaka huu no Kilimanjaro Premium Lager (mdhamini Mkuu) km 42, Tigo Km 21, Gee Soseji Km 5 wadhamini wa meza za maji Simba Cement, Kilimanjaro Water, TotalEnergies,TPC Sugar na CRDB Bank, wabia wakuu GardaWorld Tanzania, Salinero Hotel na cMC Automobiles, Wasambazaji wakuu KeysHitel na Kibo Palace Hotel.

Mbio hizi huandaliwa na Kilimanjaro Marathon Company Limited na kuratibiwa kitaifa na Executive Solutions Limited.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad