Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye mazungumzo na Mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni Mwanasiasa Maarufu wa Marekani Michael Bloomberg kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) unaofanyika Dubai, tarehe 02 Desemba, 2023. Mfanyabiashara huyo amekuwa Mdau mkubwa wa kusaidia zao la chai nchini Tanzania kwa Wanawake katika Wilaya 8 ikiwemo Lushoto, Rungwe na Korogwe. katika Mkutano wa (COP28), Chai ya Tanzania imekuwa Chai Rasmi na watu wengi wamekuwa wakiifurahia. Licha ya kuitangaza Chai ya Tanzania Kimataifa pia amesaidia kutoa msaada wa Fedha, uanzishwaji wa mnada wa Chai pamoja na Maabara ya kupima ubora wake.
Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan akipata kikombe cha Chai ya Tanzania ambayo ni Rasmi katika Mkutano wa COP 28 wakati akiwa kwenye mazungumzo na Mfanyabiashara mkubwa ambaye pia ni Mwanasiasa Maarufu wa Marekani Michael Bloomberg kando ya Mkutano wa Umoja wa Mataifa wa Mabadiliko ya Tabianchi (COP28) unaofanyika Dubai, tarehe 02 Desemba, 2023.
No comments:
Post a Comment