HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, December 3, 2023

RAIS MSTAAFU DKT. KIKWETE AONGOZA MBIO ZA UDSM MARATHON, TCAA YASHIRIKI


Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete amewaasa watanzania kufanya utaratibu wa kufanya mazoezi kuwa wa kudumu kwa kila mmoja ili kujiepusha na maradhi na kujipunguzia gharama za matibabu ya magonjwa yanayoweza kuepukika kwa kufanya mazoezi mara kwa mara.

Dkt. Kikwete amesema hayo wakati wa kuhitimisha mbio maalum kwa ajili ya kusaidia Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) yaliokuwa na lengo la Kuboresha Maisha ya Mwanachuo na kuwaweka wafanyakazi wao kuwa imara kiafya ili kuweza kukabiliana na baadhi ya magonjwa na kudumisha ushirikiano yaliyojulikana kwa jina la Udsm Marathon yenye kauli mbiu Kimbia Nasi, Boresha Maisha ya Mwanachuo zilizofanyika viwanja vya Chuo hicho Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba, 2023.

Dkt Kikwete katika mbio hizo alishiriki kwa kutembea Kilomita Tano (5KM) ikiwa ni kuimarisha afya pamoja na kuunga mkono marathon hizo ambapo wafanyakazi wa  Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) wameshiriki mbio hizo. 

Akizungumza mara baada ya Mbio hizo Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA Bw. Teophory Mbilinyi amesema wameshiriki wafanyakazi 70 wa Mamlaka hiyo ikiwa ni kuwaweka wafanyakazi wao kuwa imara kiafya pindi wanapokuwa kazini ili kupelekea ufanisi katika utekelezaji wa majukumu yao ya Mamlaka hiyo.

Mbilinyi amesema TCAA inatambua wajibu ilionao katika kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili jamii ya watanzania na hivyo kushirikiana na serikali na  kuwekeza katika masuala ya jamii ikiwemo afya, elimu, mazingira na uwekezaji kwa wanawake na vijana.

Nae Jackline Ngoda mfanyakazi wa Mamlaka ya Anga ameongezea kwa kusema mbio hizo ni muhimu kwao kwani wamekuwa na hulka ya kuaandaa mbio kama hizo hivyo inasaidia kuwajenga kiafya zaidi

Aidha Ampelius Kikoyo mfanyakazi wa Mamlaka ya Anga amesema mbio hizo zinawajenga kiafya, na kiakili hivyo mda wote kuwa imara .
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete akiongoza matembezi ya Udsm Marathon ya kilometa Tano, Mbio za kilometa Tano na Mbio za kilometa 10 wakati wa Udsm Marathon yaliyokuwa na kauli mbiu Kimbia Nasi, Boresha Maisha ya Mwanachuo yaliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba, 2023.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) pamoja na wadau mbalimbali wakiwa kwenye Matembezi na Mbio zilijulikanazo kama Udsm Marathon yaliyokuwa na kauli mbiu Kimbia Nasi, Boresha Maisha ya Mwanachuo yaliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba, 2023.
Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dkt. Jakaya Kikwete akimaliza matembezi ya kilometa Tano (5KM)  ya Udsm Marathon yaliyokuwa na kauli mbiu Kimbia Nasi, Boresha Maisha ya Mwanachuo yaliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba, 2023.
Mkurugenzi wa Huduma za Mamlaka ya TCAA Bw. Teophory Mbilinyi akiwa kwenye pich a ya pamoja na Wafanyakazi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) mara baada ya kumalizka kwa Udsm Marathon yaliyofanyika viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM)  Jijini Dar es salaam leo tarehe 03 Desemba, 2023.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad