HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 4, 2023

Taasisi ya TOAM Kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia-Hai

 
TAASISI ya Kilimohai Tanzania (TOAM) inatarajia kuzindua Mkakati wa Kitaifa wa Kilimo Ikolojia-Hai (NEOAS) unaolenga kuweka mikakati ya kuimarisha kilimohai.

Akizungumza jijini hapa, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa TOAM, Dkt Mwatima Juma alisema mkakati hiyo utazinduliwa wakati wa Mkutano wa tatu wa kitaifa wa kilimo ikolojia-hai utakaofanyika Novemba 8 hadi 9 jijini Dodoma.

Alisema TOAM inaishukuru Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kutuunga mkono wa kutengeneza Mkakati wa Kilimohai Ikolojia ambao utazinduliwa.

Dk Mwatima alisema suala la kilimohai hapa nchini bado halijaenea kwa kiwango kikubwa.
"Kwa hapa nchini kilimohai ni fursa kubwa sana kwani uzalishaji wake ni mkubwa na inapunguza gharama za kilimo kwa mkulima kutumia fedha nyingi kununua kemikali."

Alisema faida za watanzania kujikita kwenye kilimohai ni kwasababu mazaoa yake ni mkuhimu katika kulinda afya za walaji na afya ya udongo hivyo kuwa na kilimo endelevu.

Awali, Mkurugenzi wa TOAM, Bakari Mongo alisema mkutano huo unakaulimbiu ya Tunza Asili, kwa Afya Bora ukilenga kuchochea utekelezaji wa vitendo jitihada mbalimbali zilizopo kwa ajili ya kukuza sekta ya kilimo ikolojia-hai kwa kuwakutanisha wadau mbalimbali wa sekta ya kilimo.

Alisema hatua hiyo itachangia kufikia viashiria vya mpango jumuishi wa programu ya Maendeleo Afrika (CAADP) na kwa ujumla malengo la maendeleo endelevu.

Alisema washiriki katika mkutano huo ni wakulima, walaji, wafanyabaishara, wagani, watafiti, watunga sera, wataalamu wa wizara, taasisi za elimu ya juu, sekta binafasi, taasisi zisizo za kiserikali na wabia wa maendeleo.

Alisema mkutano utakuwa na wasemaji maarufu, warsha za kubadilishana uzoefu, majadiliano ya wazi na vikao vya taarifa.

"Washirika watakapa fursa ya kushirikiana na wataalamu wa sekta, kuuliza maswali na kupata uelewa wa maendeleo ya kilimo hai nchini na Afrika Mashariki."

Mkutano pia utatoa fursa kwa wakulima kuwasilisha uzoefu wao, changamoto na shuhuda za mafanikio na kutoa mapendekezo pia.

Naye Mwakilishi wa Shirika la Kilimo Endelevu Tanzania(SAT), Elizabeth Girangai alisema taasisi yake imewajengea uwezo wakulima wa kilimohai 2,700 ili kufuata kanuni bora za kilimohai na mpaka sasa wanaofuata vigezo hivyo ni zaidi ya wakulima 300 ambao wanalima ekari 1,200.

"Nitoe wito kwa wakulima kuwa Kilimo hai kinafaida kinamsaidia kupunguza gharama za kilimo, kinamsaidia kupata soko lenye tija kwa kuzalisha mazao yenye ubora kwa kiwango kikubwa hivyo kupata bei nzuri kwa soko la ndani na nje ya nchi."

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad