HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 4, 2023

WASHINDI 40 MTOKO WA KIBINGWA KUSHUHUDIA DERBY YA KARIAKOO BADO HAMJASEMA

 WASHINDI 40 Promosheni ya Mtoko wa Kibingwa kuitazama Derby ya Kariakoo kati Simba na Yanga itakayofanyika kesho kwenye uwanja wa Mkapa Jijini DaresSalaam.


Akizungumza na Wanahabari mapema Leo Novemba 04,2023 Afisa Habari wa Kampuni ya Betika Tanzania Juvenalius Rugambwa wakati akiwapokea Washindi 40 promosheni ya Mtoko wa Kibingwa Uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julias Nyerere amesema washindi hao wamepatikana kupitia droo ya mtoko Kibingwa iliyoanza Mapema Oktoba.

"Kama mnavyowaona hawa ni washindi ambao wamepatikana kupitia kampeni yetu ya mtoko kibingwa,na hawa washindi 40 waliowasili Leo wataenda kuungana na wenzao wa Dar es Salaam nakukamilisha idadi kamili ya washindi 40 na wote watakwenda kulala kwenye hoteli ya nyota tano"

"Na kesho wakiamka watakula chakula kizuri baada ya hapo watapelekwa na Ving'ora kwenye kuitaza Deby ya Simba na Yanga na watakaa VIP "Amesema Jevenalius.

Hata hivyo Jevenalius amesema kampuni ya Betika imekuwa ikitoa ushindi hapo hapo pia itaendelea kuonesha nia yao ya dhati kunyanyua michezo kuanzia mpira wa soko hadi kutoa udhamini katika michezo mbalimbali.

"Kama ambavyo tulivyo sisi mshindi akishinda anapewa zawadi zake hapohapo kwa haraka,tunawaomba watu waendelee kutupia ubashiri kwa kutembelea kwenye website yetu hata hii mechi ya Simba na Yanga ipo hapo"Amesema

Nao baadhi ya washindi hao,akiwemo Juma Makalani kutoka Mkoa Mtwara pamoja Michael Kawala kutoka Sumbawanga,wameishukuru kampuni ya Betika kuwapa fursa ya kuitazama Deby ya Simba na Yanga,kwani ilikuwa ndoto yao.

"Kweli Betika hawana longolongo ,kwa mara ya kwanza nimepanda ndege hata nilipoambiwa nimeshinda sikuamini,nawashukuru sana Betika "Amesema Kawala
Afisa Habari kutoka Kampuni ya Betika Juvenalius Rugambwa akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 04,2023 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Kuwapokea Washindi 40 wa Mtoko wa Kibingwa ambao wamepata fursa ya Kuja Kushuhudia Derby ya Kariakoo Kesho kwa Mkapa.
Mshindi wa Mtoko wa  Kibingwa na Betika Msimu wa tatu  Juma Makalani akizungumza na Wanahabari Leo Novemba 04,2023 mara baada ya Kuwasilisha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Jijini Dar es Salaam akitokea Mkoa wa Mtwara kwa ajili ya kushuhudia derby ya Kariakoo  kati ya Simba na Yanga Kesho Novemba 06,2023 Kwa Mkapa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad