HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, November 7, 2023

MLOGANZILA KUFANYA KAMBI MAALUM YA UPANDIKIZAJI NYONGA NA MAGOTI BANDIA

Hospitali ya Taifa Muhimbili-Mloganzila kwa kushirikiana na Hospitali ya Queen Elizabeth ya nchini Uingereza itafanya kambi maalumu ya upasuaji wa kuweka nyonga na magoti bandia kwa wagonjwa wenye changamoto za maradhi ya nyonga na magoti kuanzia tarehe 27.11.2023 hadi 01.12.2023.

Akielezea kambi hiyo, Daktari Bingwa wa Upasuaji Mifupa, Nyonga na Magoti, Dkt. Shilekirwa Makira amesema wagonjwa watakaonufaika na huduma hizo ni pamoja na wenye matatizo ya nyonga zilizosagika zenye maumivu makali na magoti yaliyosagika.

Dkt. Makira ameongeza kuwa watu wenye changamoto hizo watabadilishiwa kwa kuwekewa nyonga na magoti bandia kitu kitakachowafanya waondokane na maumivu wanayoyapata kabla ya nyonga zao kubadilishwa.

“Tungependa watu wajitokeze na kujisajili mapema kabla ya tarehe 27.11.2023 ili hospitali iweze kufanya maandalizi stahiki ikiwemo pamoja na kufanya vipimo vya awali ambayo ni muhimu kabla ya kufanya upasuaji huu” amesisitiza Dkt. Makira

Dkt. Makira amefafanua kuwa kwa wale waliojiunga na Mfuko wa Taifa ya Bima ya Afya, mfuko unagharimia zaidi ya asilimia 90, pia bima zingine zinagharimia matibabu haya hivyo wasisite kujitokeza kuchangamkia fursa hii adhimu.

Kwa maelezo zaidi, ushauri au kuweka miyadi (appointment) unashauriwa kuwasiliana na Madaktari Bingwa Idara ya Magonjwa ya Mifupa na ajali ambao ni Dkt. Makira simu namba 0765958302, Dkt. Abuu 0715219175 na Dkt. Amos 0683680522

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad